January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lyimo ahamasisha kilimo

Mahindi yakiwa shambani

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Suzan Lyimo (Chadema), ameibana Serikali ieleze ni lini itakuwa na chakula cha kutosha kutokana na kuwepo kwa vyanzo vingi vya maji. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Pia amehoji ni mikakati gani ambayo serikali inafanya ili kuwepo kwa utaratibu wa uvunaji wa maji ili kuimarisha kilimo cha umwagiliaji.

“Ni aibu sana kwa taifa la Tanzania kuwa na njaa wakati kuna vyanzo lukuki vya maji, mfano mzuri ni kama kule Shinyanga kuna maji mengi ambayo yakitumiwa vizuri yanaweza kusababisha kuwepo kwa kilimo cha umwagiliaji.

“Lakini pia serikali imejipangaje katika suala zima la uvunaji wa maji ya mvua ili kuhakikisha maji hayo hayapotei na yanaweza kutumika katika kilimo cha umwagiliaji,” amehoji.

Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Rachel Mashishanga (Chadema), alitaka kujua serikali inafanya jitihada gani za kuleta msaada wa chakula katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu wakati huu.

Akijibu maswali hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenister Muhagama, amesema si kweli kuwa taifa lina njaa.

Amesema “kwa sasa kuna akiba ya chakula tani lakini nne ambacho kipo katika hifadhi ya ghala la chakula la Taifa (NFRA).”

Mhagama ameongeza kuwa, serikali kila mwaka hufanya tathmini ya hali ya chakula katika wilaya na mikoa yote nchini kubaini upungufu.

error: Content is protected !!