Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Michezo Lwandamina kwenye mtihani mgumu leo
Michezo

Lwandamina kwenye mtihani mgumu leo

Prince Dube
Spread the love

KIKOSI cha Azam FC chini ya kocha, George Lwandamina kitashuka dimbani leo kuwakabili Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi majira ya saa 1 kamili usiku. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Azam FC ambayo kwa sasa haina mwenendo mzuri kwenye michezo ya Ligi Kuu mara baada ya kutopata ushindi kwenye michezo sita iliyopita, wanakwenda kuikabili Ruvu Shooting ambao wanaonekana kufanya vizuri hivi karibuni toka timu hiyo ilivyokuwa chini ya Boniface Mkwasa.

Huu utakuwa mchezo wa pili kwa Lwandamina ndani ya Azam mara baada ya kwenda sare ya mabao 2-2 dhidi ya Namungo kwenye mchezo uliopita toka alipochukua mikoba ya Aristica Cioaba aliyetimuliwa kwenye timu hiyo kufuatia matokeo mabovu.

Ruvu Shooting ni moja ya timu ambazo zimeonesha upinzani mkubwa kwenye Ligi Kuu hasa inapokutana na timu kubwa za Simba, Yanga na Azam FC.

Imekuwa timu ya pili kumfunga bingwa mtetezi klabu ya Simba wakiwa nyumbani kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika 26 oktoba 2020 kwenye Uwanja wa Uhuru na kumalizika kwa bao 1-0.

Mpaka sasa timu zote hizo zimeshacheza jumla ya michezo 15 kwenye Ligi Kuu huku Azam FC ikishinda michezo nane, Ruvu Shooting wao wakishinda michezo sita, Azam FC amekwenda sare mara nne, huku Ruvu akienda sare mara sita, na kwa pamoja timu zote zikiwa zimepoteza michezo mitatu.

Kwenye msimamo wa Ligi Azam FC inashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 28, huku Ruvu Shooting wakiwa kwenye nafasi ya nne wakiwa na pointi 24.

Kuelekea kwenye mchezo huo Azam FC itakosa huduma ya wachezaji wake wanne muhimu, ambao ni Prince Dube, Salum Abubakar, Richard Djodi na Braison Raphael.  

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

error: Content is protected !!