Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lwakatare: Ukishinda, usipotangazwa na NEC ni uzembe
Habari za Siasa

Lwakatare: Ukishinda, usipotangazwa na NEC ni uzembe

Spread the love

WILFRED Lwakatare, Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia Chadema, amekwenda kinyume na kiapo cha kustaafu siasa, kwa kurudi katika Chama cha Wananchi (CUF), alichokuwepo awali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam … (endelea).

Mara kadhaa Lwakatare alitangaza kustaafu siasa, ambapo  tarehe  14 Aprili 2020, akiwa bungeni jijini Dodoma, alisema hana mpango wa kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020, na wala hatojiunga na chama chochote cha siasa.

Lakini leo Jumamosi tarehe 30 Mei 2020, Lwakatare amerudi CUF na kupokelewa na Maftah Nachuma, Makamu Mwenyekiti wa CUF Bara, katika Ofisi Kuu za chama hicho, zilizoko Buguruni jijini Dar es Salaam.

Lwakatare amerudi CUF baada ya kuvuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kosa la kukaidi agizo la chama hicho, lililowataka wabunge wake kutohudhuria vikao vya bunge kwa muda wa siku 14.

Chadema kiliwataka wabunge wake  wajiweke karantini kama tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19).

Akitoa sababu za kwenda kinyume na msimamo wake wa kustaafu siasa, Lwakatare amesema CUF kilimuomba arudi.

 “Miaka mitatu, nilitangaza wazi hata bungeni wanafahamu nikasema mimi natarajia ifikapo Oktoba 2020 nikimaliza kipindi cha Bunge sigombei tena nataka nipumzike ili nifanye mambo mengine. Mungu ana muda wake. Nimebakiza mita chache kumaliza mbio nashtukia leo nimeinuliwa tena,” amesema Lwakatare.

Sambamba na hilo, Lwakatare amesema yeye ni miongoni mwa watu waliokiasisi chama cha CUF, hivyo amerudi ili kuhakikisha chama hicho kinaimarika, hususan kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 2020.

Akizungumzia kuhusu hatma ya ubunge wake, Lwakatare amesema yeye ni mbunge anayetambuliwa na Ofisi ya Spika wa Bunge, baada ya chama chake kumfukuza.

“Mimi nimetoka Chadema, ni mbunge anayetokana na ofisi ya spika sababu mimi chama changu kimenifukuza. Najidai sina deni na mtu, siangalii kushoto wala kulia,” amesema Lwakatare.

Lwakatare ameahidi kutumia uzoefu wake katika masuala ya uchaguzi, katika kuhakikisha CUF, kinapata ushindi.

“Mimi ni mtaalamu wa uchaguzi, nimegombea chaguzi nimeshinda na nimeshindwa . Sijawahi kushindwa kwa kura za aibu, lakini nikishinda nashinda kwa kishindo. Sikwepeshi Chadema wananijua, CCM  wananijua na hata CUF mnanijua,” amesema Lwakatare na kuongeza:

“Uchaguzi ni namba, ukipoteza mtu mmoja umepoteza kundi kubwa la watu. Sio sifa kuwa mpinzani siku zote.”

Wakati huo huo, Lwakatare ametoa msimamo wake kuhusu utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akisema kwamba ili itende haki, wanatakiwa kuja mbinu zitakazowawezesha kukwepa changamoto cha tume hiyo.

Miongoni mwa changamoto zinazolalamikiwa na vyama vya upinzani dhidi ya utendaji wa NEC, kutotangazwa kwa washindi halali wa uchaguzi.

Lwakatare amesema, yeye ana mbinu za kushinda changamoto za NEC, ndiyo maana ameweza kutangazwa mbunge na tume hiyo kwa zaidi ya mara moja, pindi aliposhinda kwenye uchaguzi.

“Sisi tumekuja bungeni si chini ya mara moja, kwa tume hii tuliyo nayo. Tuulizeni tulishindaje, tuulizeni tulitumia mbinu zipi?.  Ili anayekuja kugombea ajue mbinu na kuacha kulia kwamba tume hii sio huru,” Wilfred Lwakatare, Mbunge Bukoba Mjini.

Lwakatare amesema, wanasiasa wanaolalamika kuibiwa kura katika uchaguzi, ni wazembe.

“Maalim Seif huko Zanzibar kila siku anasema anaibiwa kura, hamjui kuibiwa ni udhaifu?  Kama uko makini na unajitambua huwezi kuibiwa,  kuibiwa ni sehemu ya uzembe na unyonge wa kutojua kuingia kwenye uchaguzi,” amesema Lwakatare.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!