Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Luteni Urio: Mbowe alinificha
Habari za SiasaTangulizi

Luteni Urio: Mbowe alinificha

Spread the love

 

SHAHIDI wa Jamhuri, katika kesi yenye mashtaka ya ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, Luteni Denis Urio, amedai mwanasiasa huyo alimficha kuhusu majina ya vituo vya mafuta, alivyopanga kuvilipua. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Luteni Urio ametoa madai hayo leo Ijumaa, tarehe 28 Januari 2022, akiulizwa maswali ya dodoso na Wakili wa utetezi, Dickson Matata, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar ea Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, waliokuwa makomando wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Wanashtakiwa kwa mashtaka sita ya ugaidi, ikiwemo kupanga kudhuru viongozi wa Serikali, kulipua vituo vya mafuta na maeneo yenye mikusanyiko ya watu, katika majiji ya Mwanza, Arusha na Dar ea Salaam. Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Julai hadi Agosti 2020.

Wakili Matata alimhoji Luteni Urio kama ifuatavyo;

Matata: Tukisema tutajie vituo ambavyo ulisema alipanga kulipua Mkoa wa Mwanza utakuwa na majibu au hutakuwa na majibu?

Shahidi: Majibu anayo Mbowe, mimi sitakuwa na majibu hayo.

Matata: Nakuuliza wewe kuhusu simulizi ya Mbowe, ukiulizwa vituo vya mafuta alivyotaka kulipua Mwanza utakuwa na majibu au hautakuwa na majibu?

Shahidi: Mimi majibu hayo sina, atakuwa nayo Freeman Mbowe.

Matata: Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa na hivyo vituo au hautakuwa navyo?

Shahidi: Majibu hayo mimi sina anayo Mbowe, alinificha kuniambia.

Matata: Ukiulizwa ni sehemu ipi ipo specific alipanga kukata miti kwenye barabara ya Morogoro na Iringa, utakuwa na majibu au hauna?

Shaiidi: Kati ya Barabara ya Morogoro na Iringa hakuniambia specific ni maeneo gani.

Matata: Ulitaja viongozi wengine wa upinzani alipanga kuwashambulia?

Shahidi: Sikutaja viongozi wowote ila aliniambia viongozi wa Serikali ambao ni vikwazo kwa vyama vya upinzani.

Matata: Hapana shaka mpaka anakushirikisha alikuwa anakuamini, kweli si kweli?

Shahidi: Ni sahihi.

Matata: Tukiachana na suala la kukwambia umtafutie hao vijana, kuna chochote alikueleza mfano kumtafutia vilipuzi kwa ajili ya kulipulia hayo masoko?

Shahidi: Hakunieleza.

Matata: Alikuambia kuhusu kumtafutia silaha kuwadhuru hao viongozi wanaozuia upinzani?

Shahidi: Hakunieleza.

Shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!