Thursday , 13 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100
Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote juu ya muda wa miaka 100 wa uwekezaji kwenye Bandari ya Dar es Salaam kupitia Kampuni ya DP World kutoka Falme za Kiarabu kama inavyoenezwa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kauli hiyo ya Lissu imekuja siku moja baada ya kuibuka mjadala kuhusu uwepo wa mkataba wa kampuni hiyo kwamba inatarajiwa kuwekeza bandarini kwa miaka 100 – jambo ambalo limezua taharuki.

Akizungumza na Mtandao wa Chanzo Kikuu leo Jumatano, Lissu ambaye pia ni mwanasheria mbobevu amesema; “Wakati huu ambao Chadema itatoa taarifa kuhusiana na sakata hili, mimi kwa maoni yangu binafsi nasema kuwa sijaona mahali popote kunapoonyesha kuwa Kampuni ya DP World wamepewa ofa ya miaka 100 ya kuendesha Bandari yetu,” alisema Lissu.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini Tanzania (TPA), jana Jumanne usiku walilazimika kutoa taarifa kwa Umma, juu ya uwapo wa kikundi cha watu walioamua kwa makusudi kupotosha kuhusiana na mchakato wa maboresho ya Bandari nchini yenye lengo la kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Spread the loveChama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP)...

BiasharaHabari za Siasa

Prof. Mkumbo: Pato la taifa limefikia trilioni 148

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mwaka...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Deni la Serikali lafikia trilioni 91

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Dk. Shogo Mlozi afariki dunia

Spread the loveMbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambaye pia ni...

error: Content is protected !!