January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lusinde akumbana na nguvu ya UKAWA Mwanza

Spread the love

MBUNGE wa Jimbo la Mtela (CCM), Livingstone Lusinde amejikuta katika wakati mgumu baada ya wananchi na wanaccm, kumtaka atelemke kutoka jukwaani kwa kile walichodai hazungumzi vitu vya msingi. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kasheshe hiyo alikumbana nayo juzi wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi mkoa wa Mwanza, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani jijini hapa.

Wananchi `kiduchu` waliofika katika mkutano huo walisikika wakikipiga kelele kushinikiza Lusinde kutelemka kutoka jukwaani kwa madai hana cha kuzungumza huku wengine wakisema hawana imani na CCM.

Wananchi hao walisikika wakisema, “hivi Lusinde badala ya kuzungumza kitu na mipango yenu na nini mtawafanyia watanzania kazi yako ni `upuuzi` na kuzungumzia vyama vya upinzani? Kama CCM hamna cha kutuambia ni bora Nchi muwaachie UKAWA.”

Hata hivyo Lusinde anayesifika kwa kuporomosha mvua ya matusi, alionekana kushindwa kuhutubia kutokana na wananchi wachache waliojitokeza kwenye mkutano na badala yake alianza kuviponda vyama vya upinzani.

Lusinde katika mkutano huo alitumia dakika 45 kumzungumzia mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Katika hatua nyingine wananchi wachache hao waliofika kwenye mkutano huo walisikika tena wakisema, “CCM na watu wake hatuwataki hapa Mwanza ondokeni na wala hapa hatutaki kuona jezi ya rangi kijani na Njano.”

Mmoja wa Wananchi aliyejitambulisha kwa jina moja la Daud alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi, kwanini hawaitaki CCM Mwanza amesema: “Hata wewe mwandishi unafahamu CCM ambavyo wamelingiza Taifa hili katika umasikini na wananchi wake kuwa masikini, wengi wetu hapa tulipo hata `buku` ya kununua unga kuipata ni shida.”

Daud amesema kitendo cha timu ya kampeni ya CCM, yenye watu 32, wakiwamo, Harrison Mwakyembe, Makongolo Nyerere, Mwiguru Nchemba na Ummy Mwalimu kwamba ni watu wasiokuwa na staha na ushawishi kwa watu.

Akitolea mfano wa Lusinde wakati akihutubia mkutano huo, amesema ameshindwa kujenga hoja na kuwaeleza Watanzania ni nini mgombea wao na CCM walivyojipanga kuwatatulia wananchi kero, badala yake anaropoka.

Hata hivyo baada ya Lusinde kuona wananchi hao kuanza kupinga poroja zake alianza kuwanadi wagombea ubunge wa CCM katika majimbo mawili ya Nyamagana na Ilemela.

Lusinde katika kuwanadi wagombea hao amesema, “Wananyamagana mlikosea wenye kuwachagua wabunge wa Nyamagana na Ilemela hivyo basi mnapaswa kuwachagua, Stanslaus Mabula na Angelina Mabula (wagogombea ubunge Nyamagana na Ilemela) kwa maendeleo ya wananyamagana.”

error: Content is protected !!