Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Michezo Lulu atambulisha jina la mwanae, amwandikia ujumbe
Michezo

Lulu atambulisha jina la mwanae, amwandikia ujumbe

Elizabeth Michael 'Lulu'
Spread the love

 

MSANII wa maigizo nchini Tanzania, Elizabeth Michael maarufu Lulu amemwandikia ujumbe mwaanae mwenye siku 21 akichambua jina alilompa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lulu alifunga ndoa na mfanyabiashara na mmiliki wa kituo cha habari cha EFM, Francis Ciza maarufu Majjizo tarehe 16 Februari 2021 katika Kanisa Katoliki la Mt. Maximilian Maria Kolbe, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Wawili hao, walibahatika kupata mtoto wa kiume, tarehe 16 Julai 2021 na kuujulisha umma huku wote kila mmoja kwenye kurasa zao za kijamii walisema mtoto huyo anaitwa G.

Usiri wa kirefu cha G ulitawala na maswali ya hapa na pale yalikuwapo kutaka kujua G ina maana gani.

Leo Ijumaa, tarehe 6 Agosti 2021, kupitia ukurasa wa Instagram, Lulu amelitambulisha jina rasmi la mwanae huyo likiambatana na ujumbe aliosema, akikuka atakuja kuusoma kwani teknolojia ina hifadhi.

Lulu amesema, mwanae anaitwa Genesisi.

Ujumbe wote wa Lulu kwenda kwa mwanae huyo huu hapa chini;

Name is GENESIS means BEGINNING (MWANZO) πŸ˜‡

Genesis,

Najua kuna siku utakuwa Na utasoma huu ujumbe (wanasema teknolojia/intaneti haisahau…😊)

Mara zote ukisoma huu ujumbe ukukumbushe maana ya jina lako…iliyobeba maana halisi ya maisha yako kwa machache tuliyofunuliwa sisi wazazi wako na mengine mengi utaendelea kufundishwa na ROHO WA MUNGU kadiri ya unavyo endelea kukua.

Kama lilivyo jina lako GENESIS yaani MWANZO…WEWE ni MWANZO wa kila lililo JEMA….Neno La MUNGU linavyoonyesha kitabu cha MWANZO 1:3….MUNGU alivyoamuru iwe NURU kabla ya kuanza kitu chochote MWANZOni kabisa katika uumbaji….basi vivyo hivyo;

*Ukawe MWANZO wa NURU kila penye giza.
*Ukawe MWANZO wa FURAHA kila penye huzuni.
*Ukawe MWANZO wa AMANI kila penye ugomvi.
*Ukawe MWANZO wa KICHEKO kila penye kilio.

Yaani, ukawe MWANZO wa kila lililo JEMA kwenye maisha ya watu waliokuzunguka na watu wote watakao bahatika kukutana na wewe….!

Kwetu kama familia…Umekuwa MWANZO wa furaha mpya Na mengi mazuri πŸ’™Najua utaweza kuwa yote hayo na hata zaidi….Kwasababu najua MUNGU ALIKUJUA na KUKUTAKASA hata kabla ya KUKUUMBA na kabla ya kukutoa katika TUMBO LANGU (Yeremia 1:5)WEWE NI MWANZO….na MWANZO haujali KWANZA.
GENESIS sio jina tu….GENESIS ni DENI lako mwanangu….Kua Ukalilipe DENI hili..!

Nifanye Nijivunie wewe…Zifanye MBINGU zijivunie wewe πŸ™
Ubarikiwe….Nakupenda ❀️

With Love,

Mama G πŸ’™

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!