Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lukuvi sasa kutembea mkoa kwa mkoa
Habari za Siasa

Lukuvi sasa kutembea mkoa kwa mkoa

Spread the love

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameamua kutembea mkoa kwa mkoa ili kukabili migogoro ya ardhi nchini. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Leo Alhamisi tarehe 22 Novemba 2018 atafanya ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika shamba la Singu na Endasagu yaliyopo Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara ili kutatua migogoro katika mashamba hayo baina ya wamiliki na wananchi.

Uamuzi wa Lukuvi kufanya ziara katika mashamba hayo ni moja ya jitihada zake za kushughulikia migogoro ya ardhi kutokana na uwepo kero na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusiana na huduma za ardhi.

Akiwa wilayani Babati, Lukuvi atakagua mashamba ya Singu na Endasagu sambamba na kusikiliza malalamiko ya wananchi kuhusiana na mashamba hayo na baadaye kutafuta ufumbuzi.

Aidha, katika mfululizo wa kushughulikia migogoro ya ardhi, Lukuvi mara baada ya kurejea kutoka mkoani Manyara atafanya ziara katika halmashauri zote za mkoa Dar es Salaam,Wilaya za Kinondoni, Ilala, Kigamboni, Ubungo na Temeke ambapo mbali na mambo mengine atakagua na kuhamasisha zoezi la urasimishaji ambalo limeonekana kuwa na changamoto katika baadhi ya maeneo.

Vile vile, katika kuhakikisha migogoro ya ardhi inapungua nchini Lukuvi mwanzoni mwa mwezi Desemba atakuwa na ziara ndefu itakayohusisha mikoa ya Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa na Pwani ambapo wananchi watapata fursa ya kuwasilisha kero za ardhi kupitia programu ya ‘Funguka kwa Waziri.’

Ziara hiyo ni muendelezo wa ziara zake za kushughulikia migogoro ya ardhi ikiwa ni baada ya kutoka mkoani Kilimanjaro ambapo alitatua migogoro ya ardhi ikiwemo ya mashamba makubwa katika Wilaya za Hai, Moshi na Same.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!