Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lukuvi atishia kumtoboa kitambi DED
Habari za Siasa

Lukuvi atishia kumtoboa kitambi DED

William Lukuvi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Spread the love

WILLIAM Lukuvi, WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Makazi, amemtahadhalisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, John Wanga, kwamba atakitoa pumzi kitambi chake, endapo atashindwa kusimamia zoezi la Urasimishaji makazi holela, anaandika Moses Mseti.

Lukuvi amesema kwamba zoezi la urasimishaji makazi holela linaloendelea nchini kote kwa mkoa wa Mwanza na halmashauri hiyo lilitakiwa kukamilika Januari mwaka huu lakini mpaka sasa zoezi hilo halijakamilika.

Amesema kuwa, ameshangaa kuona Mkurugenzi huyo pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Leonard Masale wakishindwa kusimamia zoezi hilo na kusababisha kuendelea kuwepo kwa makazi holela licha ya halmashauri hiyo kuwa na watumishi wengi.

Lukuvi amesema kwamba Halmashauri hiyo ilitakiwa iwe imepima na kutoa hati ya viwanja 35, 000 ambavyo vingelipiwa kodi ya Sh. 2.3 bilioni lakini halmashauri hiyo imesajili na kupima viwanja 834 pekee navyo hawajakusanya kodi na kudai kwamba ni sawa na kazi bure.

Pia amesema kuwa, halmashauri hiyo katika kumbukumbu ya awali waliomsomea walikusudia kupima viwanja hivyo, 35,000 lakini msijala rekodi inaonesha vinavyotakiwa kupimwa ni 28,000 hivyo viwanja 700 havionekani vilipo.

“Alafu nyie hapa mna Mkurugenzi wenu mjanja sana, lakini kazi yenyewe ndio hii, angalia sana kitambi chako tutakitia pancha na kama mtaendelea hivi lazima hatua zitachukuliwa mara moja na hatutokubali kuikosesha mapato Serikali.

“Nyie hapa mna watumishi wa ardhi zaidi ya 40 lakini kazi haiendi kabisa, mnashindwa na mji mdogo wa Bunda (Mara) wenye afisa ardhi mmoja lakini wanafanya kazi vizuri na wametoa hati nyingi lakini nyie hakuna mnachokifanya,” amesema Lukuvi.

Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Isimani mkoani Iringa, ametoa siku 60 kwa Mkurugenzi huyo pamoja na mkuu huyo wa wilaya kuhakikisha ifikapo 30 Juni zoezi la urasimishaji makazi holela mkoa wa Mwanza liwe limekamilika na kwamba halmashauri itakayoshindwa hatua zitachukuliwa.

Amesema kuwa muda huo ukifika kama bado watu hawajalasimisha makazi yao hakuna kiwanja kitakachojengwa na kwamba utafuatwa mfumo mpya wa master plan ambao unatarajia kuanza Agousti mwaka huu unaolenga nyumba zinazotakiwa kujengwa ni zile viwanja vyao vimepimwa.

Amesema kuwa watu ambao hawakubaliana na mpango huo mpya wa urasimisha makazi holela, wanapaswa kwenda vijijini ambako hakujapimwa na kwamba nyumba ambazo hazina hatimiliki zinasababisha Serikali kukosa kodi ya majengo hivyo ni lazima kila mmoja apimiwe ardhi.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, John Wanga, amesema muda huo ukifika watahakikisha wawe wamekamilisha zoezi la urasimishaji makazi holela huku akiwatuhumu watendaji wake wa Ardhi kwa kushindwa kujibu maswali ipasavyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!