March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lukuvi atangaza kubadilisha hati za ardhi 2018

William Lukuvi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Spread the love

WAZIRI wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemtaka Mkurugenzi wa Tehama katika wizara hiyo, ifikapo 2018, mradi wa mfumo unganishi wa taarifa za ardhi katika mtandao uwe umekamilika, anaandika Angel Willium.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Lukuvi amesema amesema ifikapo mwakani inatakiwa kuzinduliwa na kuanza kazi.

“Mkurugenzi hakuniambia ni tarehe ngapi kazi itakamilika, hivyo ifikapo mwakani tarehe moja mwezi wa sita, mfumo huu utazinduliwa na uanze kufanya kazi, hati mpya itaanza kutolewa na wale wenye hati za zamani watabadilishiwa amesema Lukuvi.

Aidha, Mkurugenzi wa Tehama wa wizara hiyo, Shaban Pazi amesema mfumo unganishi wa kutunza taarifa katika mtandao, kwa sasa ndiyo wanauandaa na wataanza na mkoa wa Dar es Salaam katika wilaya ya Kinondoni na Ubungo na kufatia mikoa yote ya Tanzania.

Pazi amesema lengo la mradi ni kuimarisha usalama katika umiliki wa ardhi, kutoa huduma nafuu na sahihi kwa wateja, kupunguza muda wa kuhakiki na kuhamisha ardhi, kuzuia uvamizi wa misitu, hifadhi za barabara na sehemu zilizokuwa wazi na kupunguza rushwa katika malipo.

Mradi huo ulianza mwezi Julai 2016 na unadhaminiwa na benki ya Dunia.

error: Content is protected !!