October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lukuvi amtuliza Prof. J

Spread the love

JOSEPH Haule (Prof. Jay) Mbunge wa Mikumi (Chadema), ametaka kujua ni lini serikali itafuta umiliki wa mashamba pori ya muda mrefu ya Mauzi Estate, Miyombo Estate, Sumagro Estate Kisanga Estate (Lyori Estate)?. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Mashamba hayo yapo kwenye Kata za Tindiga, Masanze, Kilangali na Kisanga na kwamba, ni lini watayagawa kwa wananchi wanyonge ili waweze kupata maeneo ya shughuli zao mbalimbali za maendeleo.

Akijibu swali hilo William Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema, serikali ya awamu ya tano imeendelea kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wote wa ardhi nchini, ambao wameendelea kukiuka masharti ya kumiliki ardhi.

Amesema, ni kutokana na kutoendeleza ardhi kwa mujibu wa sheria na taratibu, kuendeleza ardhi kinyume na masharti ya umiliki na kutolipa kodi ya pango la ardhi.

“Kwa upande wa mashamba, katika kipindi cha kuanzia Disemba, 2015 mpaka sasa, jumla ya milki za mashamba 45 zimebatilishwa katika maeneo mbalimbali nchini. Kwa mkoa wa Morogoro, jumla ya mashamba 15 yamebatilishwa ambapo mashamba 10 kati ya hayo yapo katika Wilaya ya Kilosa.

“Wizara yangu iliunda timu ya kupitia mashamba yote yaliyobatilishwa katika mkoa wa Morogoro pamoja na kukagua mashamba yenye sifa za kubatilishwa.

“Mashamba ya Mauzi Estates, Sumagro Estates, Kisanga Estates na Miyombo ni miongoni mwa mashamba ambayo timu yangu iliweza kuyakagua na hatua za ubatilisho wa milki zinaendelea,” amesema na kuongeza:

“Jumla ya mashamba yaliyokaguliwa na kupendekezwa kubatilishwa ndani ya Mkoa wa Morogoro ni 23, na yote yapo katika Wilaya ya Kilosa. Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imeelekezwa kufanya taratibu za ubatilisho kwa mashamba hayo.”

Lukuvi ametoa rai kwa halmashauri zote nchini ikiwemo

Kilosa ambazo zimebaini kuwepo kwa mashamba yasiyoendelezwa katika maeneo yao, kuwasilisha Wizarani mapendekezo ya kubatilisha milki za mashamba husika ili taratibu za kuyabatilisha zikamilishwe kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi (Sura

113)” Alisema Lukuvi.

error: Content is protected !!