October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lukuvi amteua Polepole ujumbe Bodi ya NHC

Spread the love

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameteua wajumbe saba wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa kwa umma iliyotolewa tarehe 20 Mei 2019 na Lukuvi imewataja wajumbe hao wapya akiwemo, Immaculate Senje, Sauda Msemo, Martine Madekwe, Mhandisi Mwita Rubirya, Abdallah Mwinyimvua  na Charles Singili.

“Kwa mamlaka niliyopewa chini ya Aya ya 1 (1) (b) ya Jedwali lililoanzishwa chini ya kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Shirika la Nyumba la Taifa sura 295, nimewateua wajumbe wa bodi kuanzia leo tarehe 20 Mei 2019,” inaeleza taarifa ya Lukuvi.

Waziri Lukuvi amefanya uteuzi huo kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa Dk. Sophia Kongela uliofanywa na Rais John Magufuli hivi karibuni.

error: Content is protected !!