October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lukuvi aanika aliyoyafanya ardhi toka 2014

Wiliam Lukuvi, aliyekuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Jamii

Spread the love

 

ALIYEKUWA Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema miongoni mwa kazi kubwa alizozifanya tangu aliposhika wadhifa huo 2014, kukomesha vitendo vya matajiri na wenye madaraka kupora ardhi za wananchi wanyonge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Mbunge huyo wa Isimani (CCM), ameyataja mafanikio hayo leo Alhamisi, tarehe 17 Februari 2022, akimkabidhi ofisi mrithi wake, Dk. Angelina Mabula, aliyeteuliwa na Rais Samia kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, hivi karibuni.

“Wakati tunaingia 2014 tulikuwa na mambo mengi hapa, hata mheshimiwa Jakaya Kikwete (Rais wa wakati huo), alivyoniteua kuna mambo mengi alikuwa ameniambia. Lakini wakati ule kulikuwa na malalamiko makubwa ya dhulma katika wizara hii, tumeshirikiana angalau kukomesha dhulma Kwa taratibu mbalimbali,” amesema Lukuvi na kuongeza:

“Wananchi wengi walikuwa wanadhulumiwa ardhi yao na watu wenye pesa na madaraka, lakini tumejitahidi kupunguza angalau sasa hata malalmiko hayo yamepungua.”

Kwa upande wake Dk. Mabula, ameahidi kuendeleza pale alipoishia Lukuvi, ili kuendelea kuimarisha utendaji wa wizara hiyo katika kuwahudumia wananchi.

“Haya yote ambayo umeyazungumza tumeyafanya tukiwa pamoja, naomba nikuthibitishie tutayaendeleza. Kwa sababu ndiyo yaliyobadilisha sura ya wizara. Ilikuwa kwenye Bunge tukiingia wizara ya ardhi ni siku tatu lakini imefikia mahali mpaka nusu siku kazi inakuwa imekwisha,” amesema Dk. Mabula na kuongeza:

“Nitaomba Mungu anijaalie pamoja na timu hii tusirudi kule nyuma, mnapangiwa siku mbili au tatu za wizara. Kipi kinajadiliwa? Maana yake huku mtakuwa mmetekeleza kwamba sasa baada ya Lukuvi kutoka kuna mambo hayaendi sawa matokeo yake tunarudi tulikotoka.”

error: Content is protected !!