July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lugola, Mwambalaswa, Murad huru

Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Spread the love

TUHUMA za kuomba rushwa zilizokuwa zikimkabili wabunge Kangi Lugola, Victor Mwambalaswa na Murad Sadiq zimefutwa, anaandika Faki Sosi.  

Wabunge hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuomba rushwa ya Sh.30 milioni Mbwana Magotta, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Gairo.

Lugola ni Mbunge wa Mwibara, Mwambalaswa (Lupa) na Sadiq (Mvomero) ambapo Mganga Buswau, mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (Takukuru) alifuta mashitaka hayo mbele ya Respecious Mwijage, Hakimu Mkazi katika Mahakama hiyo.

Mpare Mpoki, wakili wa utetezi ameomba maelezo ya mlalamikaji (Jamhuri) katika shauri hilo ambapo mahakama imekataa ombi hilo kutokana  na kuwa, haina uwezo wa kisheria.

Lugola akizungumza nje ya mahakama hiyo amedai kuwa, mashtaka hayo ni miongoni mwa njama za kisiasa zenye lengo la kumchafua.

“Tumeanza na Mungu na tumemaliza na Mungu. Leo tumeachwa huru, tunawaambia Watanzania kesi hiyo ni ya kutunga.

“Serikali na Takukuru wamekuwa kama vinyonga ambapo walidai kwamba, upelelezi umekamilika lakin leo wao wenyewe wamefuta kesi hiyo,”amesema Lugola na kuongeza;

“Kwa kweli tumechukizwa na udhalilisha uliofanywa na Takukuru juu yetu.”

Awali, watuhumiwa hao walidaiwa kufanya kosa hilo tarehe 15 Machi mwaka huu katika Hotel ya Golden Tulip, Dar es Salaam majira ya saa mbili hadi nne usiku wakiwa kwenye Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa.

Washtakiwawalidaiwa kuomba rushwa ili watoe mapendekezo mazuri kuhusu hesabu ya fedha za bajeti ya mwaka 2015/2016 za halmashauri hiyo.

error: Content is protected !!