KANGI Lugola Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, amemuweka ndani Ibrahim Mhando, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS) kwa kosa la kutowaweka mahabusu watu wanne wanaotuhumiwa kumpa taarifa ya uongo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Waziri Lugola ametoa agizo hilo asubuhi ya leo tarehe 27 Agosti, 2018 alipotembelea kituo hicho kwa kushtukiza, kwa ajili ya kuthibitisha utekelezwaji wa agizo lake alilolitoa jana la kuwekwa mahabusu Benjamin Kasiga Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects na wenzake kwa kosa la kutoa taarifa ya uongo kuhusu ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji Mtwara.
Alipotembelea kituo hapo, Waziri Lugola alimkuta Mhandisi Kasiga akiwa chumba cha upelelezi badala ya kuwekwa mahabusu ya polisi hiyo.
Kabla ya kuwekwa mahabusu, OCD Mhando alisema hakutekeleza agizo hilo kutokana na mahabusu ya kituo hicho kujaa watuhumiwa.
Hata hivyo, utetezi huo ulipingwa na Waziri Lugola akisema kuwa nafasi ya kukaa watuhumiwa ilikuwepo na kwamba wote wanne wangeweza kukaa bila tatizo lolote.
Leave a comment