February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lugola achemka, JPM atumbua

Kangi Lugola, Waziri wa mambo ya Ndani. Picha ndogo wakati akiapishwa

Spread the love

LICHA ya maelezo na maelekezo ya mara kwa mara yanayotolewa na Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Jeshi la Polisi, polisi wake wameendelea kuogelea kwenye tuhuma nzito. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Lugola amekua akitembelea maeneo mbalimbali nchini na kukutana na ‘vijana wake’ huku akitoa maelezo na kuonya watakaojihusisha na vitendo vya rushwa, unyanyasaji na ubambikiaji kesi lakini bado vitendo hivyo vinaendelea kumea kwenye jeshi hilo huku akishindwa kubaini.

Hatua hiyo imemsukuma Rais John Magufuli kuagiza kusimamishwa kazi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kyerwa, Justine Joseph.

Wengine wanaotakiwa kusimamishwa ni Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kyerwa, Everist Kivuyo na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kyerwa, Robert Marwa kutokana na hujuma.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu usiku wa kuamkia leo imeeleza kuwa, viongozi hao wa Jeshi la Polisi katika wilaya hiyo wanatuhumiwa kuhusika katika magendo ya zao la kahawa.

“Rais amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jeneral Jacob Kingu na Inspekta Generali wa Polisi, Simon Sirro kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanyika na hatua stahiki zinachukuliwa endapo watabainika,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Tuhuma hizo zimebainika juzi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa ziarani wilayani humo.

error: Content is protected !!