Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Lugha ya Kichina yasababisha mgomo kampuni ya ujenzi
Habari Mchanganyiko

Lugha ya Kichina yasababisha mgomo kampuni ya ujenzi

Spread the love

MGOMO wa wafanyakazi zaidi ya 290 wa Kampuni ya Kimataifa ya Geo Engineering ya China inayotekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara ya Sanya Juu hadi  Elerai kwa kiwango cha lami umetikisa mkoa wa Kilimanjaro, anaandika Mwandishi Wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu amethibitisha kuwa wafanyakazi hao wamegoma wakilalamikia mikataba yao ya ajira kuandikwa kwa lugha ya Kichina na mingine kwa Kiingereza, badala ya Kiswahili.

Kufuatia hali hiyo, amelazimika kukutana na uongozi wa kampuni hiyo na wawakilishi wa wafanyakazi hao na kutoa maelekezo ya kurekebishwa kwa changamoto hizo, huku akiwasihi wafanyakazi kuendelea na kazi wakati suala hilo likitafutiwa ufumbuzi.

“Serikali tumeshakutana nao tayari na hao viongozi wa kampuni inayotekeleza mradi huo na kutoa maelekezo ya kurekebishwa kwa changamoto hiyo ya mikataba. Lakini pia tumewaonya wafanyakazi au mtu yeyote asithubutu kuwashawishi wafanyakazi wagome au kushinikiza kuungwa mkono, watakiona chamtemakuni,”amesisitiza.

Ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 32.2 za lami zinazojengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 52.19 unatarajiwa kukamilika Oktoba 15, mwaka 2018.

Barabara hiyo inatajwa kuwa mkombozi kwa wananchi wa Wilaya ya Siha, kwa vile ndiyo injini ya kuchochea uchumi wa mkoa wa Kilimanjaro na inayoimarisha sekta ya uchukuzi na biashara kati ya mataifa ya Tanzania na Kenya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!