Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lugangira ataka usawa kijinsia Sheria Vyama vya Siasa, Uchaguzi
Habari za Siasa

Lugangira ataka usawa kijinsia Sheria Vyama vya Siasa, Uchaguzi

Mbunge wa Viti Maalum CCM, Neema Lugangira
Spread the love

 

MBUNGE wa Viti Maalum CCM, Neema Lugangira ameshauri Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Uchaguzi kupitiwa upya ili kuleta usawa wa kijinsia. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea)

Lugangira amesema hayo jana Alhamisi tarehe 14 Julai, 2022, baada ya kutoa maoni kwa Kikosi Kazi cha Rais Samia Suluhu Hassan kinachoshughulikia masuala ya demokrasia yaliyoibuliwa kwenye kikao cha wadau kilichofanyika Disemba 15 hadi 17 mwaka jana, jijini Dodoma.

Amesema amelazimika kuwasilisha maoni hayo katika eneo namba nne la kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa kutokana na ukweli kuwa kuna ombwe kubwa.

Mbunge huyo amesema amekiambia kikosi kazi kuhusu changamoto zilizopo kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Uchaguzi ili ziweze kufanyiwa marekebisho na kuendana na wakati wa sasa.

“Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Uchaguzi ni muhimu sana katika kufanikisha lengo la usawa ila kwa sasa haina meno. Mfano Sheria ya Vyama vya Siasa haimpi meno Msajili kufuatilia uwepo wa asilimia fulani ya wanawake ndani ya vyama, hivyo kinachotokea ni utashi wa vyama pekee,” amesema.

Mbunge huyo amesema iwapo Sheria itampa meno Msajili anaweza kuhoji pale ambapo vyama vitashindwa kutekeleza dhana ya usawa wa kijinsia.

Amesema Katiba inaelekeza uwakilishi wa wanawake ni asilimia 30 ya wabunge wa viti maalum lakini sheria ipo kimya jambo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa kina na sheria kuweka kiwango mahususi.

Lugangira ametolea mfano katika Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji kuwa uwakilishi wa wanawake ni asilimia 2 hali ambayo inaonesha wanawake bado ni wachache.

Kuhusu Sheria ya Uchaguzi mbunge huyo amesema ni wakati muafaka wa kutambulika makosa ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake.

“Sheria ya Uchaguzi iliyopo haitambui makosa ya ukatili wa kijinsia kama moja ya makosa ambayo mgombea anaweza kupinga mgombea mwenzake, haya yote yanahitaji kuangaliwa upya,” amesema.

Amesema pia Sheria hiyo haijafafanua ni namna gani mgomnea akitolewa lugha za kuejeli anaweza kuwasilisha, lakini pia mchakato wa kusikiliza huwa unachukua muda mrefu.

Lugangira ameshauri pia uundwaji wa kamati za maadili kuzingatia jinsia ili kuwawezesha wanawake kusikilizwa na watu ambao wanahisi kilichofanyika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!