Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko LSF yajinoa kampeni msaada wa kisheria ya Mama Samia
Habari Mchanganyiko

LSF yajinoa kampeni msaada wa kisheria ya Mama Samia

Spread the love

SHIRIKA la Huduma za Kisheria (LSF), limeanza kujipanga namna ya utekelezaji wa Nguo Kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Shirika hilo limeketi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, ikiwa siku chache tangu kampeni hiyo izinduliwe na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro, tarehe 15 Februari 2023.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala, amesema shirika lake linajipanga kutekeleza kampeni hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo kwa uratibu wa Wizara ya Katiba na Sheria itasaidia kuongeza upatikanaji wa haki nchini.

“LSF kwa takribani miaka 11 sasa tumekuwa tukitekeleza mradi wa upatikanaji haki kwa kuwezesha watoa huduma zaidi 4,000 na mashirika 184 Tanzania Bara na Zanzibar, kutoa msaada kwa watanzania wenye uhitaji bure,” amesema Ng’wanakilala.

Ng’wanalilala amesema huduma ya msaada wa kisheria imesaidia kupunguza migogoro inayokwenda mahakamani kwa kuwa asilimia 60 kati ya mashauri 90,000 yanayoletwa kwa watoa msaada wa kisheria hutatuliwa.

Ng’wanakilala amesema kuwa “tunajengea uwezo watoa huduma za msaada wa kisheria kwa kuwapatia kozi mbalimbali za kisheria na haki. Pia, tunajenga mifumo ya utawala bora, uendeshaji wa kiprogramu na usimamizi wa kifedha kwa mashirika yanayopokea ruzuku kutoka kwetu.”

“Tuko katika kampeni hii ikiwa ni sehemu ya kufikia matarajio yetu ya kuona kwamba wananchi wanajua haki zao, kunakuwa na mifumo thabiti na uboreshaji wa ushirikiano wa wadau kwa kuchochea juhudi za makusudi kuchukuliwa ili kuboresha sekta ya msaada wa kisheria nchini ikiwemo serikali kutenga rasilimali fedha kupitia mfuko wa huduma za msaada wa kisheria, ambao utafanya huduma hizi kuwa endelevu” amesema Ng’wanakilala.

Ng’wanakilala ambaye Makamu Mwenyekiti wa kampeni hiyo, Ng’wanakilala ameomba wadau wote katika sekta ya msaada wa kisheria ikiwemo Serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau wa maendeleo, sekta binafsi, pamoja na vyombo vya habari kuunganisha juhudi zao kwa pamoja katika kampeni ili kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya msaada wa kisheria na maisha ya jamii kwa ujumla hususani wanawake na watoto.

“Tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali na wadau katika kuhakikisha tunawafikia watu wengi zaidi hususani maeneo ya pembezoni.” amesisitiza Ng’wanakilala.

Kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ilizinduliwa mnamo tarehe 15 Februari 2023, ambapo itaendeshwa kwa takribani miaka mitatu nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!