November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

LSF, wadau wajadili utekelezaji programu za upatikanaji haki

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng'wanakilala

Spread the love

 

WADAU zaidi ya 200, kutoka katika Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), yanayoshughulika na utoaji huduma za msaada wa kisheria, wamefanya tathmini juu ya utekelezaji wa programu ya upatikanaji haki nchini ya Shirika la Legal Service Facility (LSF). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es salaam … (endelea).

Wadau hao wamefanya tathmini hiyo, katika mkutano wa siku mbili, ulioandaliwa na LSF na kufanyika jijini Dodoma, kuanzia tarehe 20 hadi 21 Oktoba mwaka huu.

Katika mkutano huo uliohusisha wadau hao kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, walijadili kuhusu matokeo ya programu ya upatikanaji haki ya LSF, iliyozinduliwa na Msajili wa NGO’s Tanzania, Vickness Mayao, tarehe 20 Agosti 2021.

Pamoja na maandalizi ya utekelezaji mpango mkakati mpya wa LSF wa miaka mitano unaotarajiwa kuanza 2022 hadi 2026.

Akifungua mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria kutoka Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi, na Utawala Bora Visiwani Zanzibar, Hanifa Ramadhan Said, amesema mkutano huo ni muhimu kwa kuwa unalenga kutafuta suluhu za changamoto ya upatikanaji haki nchini.

“Mkutano huu ni muhimu kwa wadau wa sekta ya msaada wa kisheria, kumekuwa na tabu mbalimbali katika jamii ambazo husababishwa na ukandamizaji wa haki, ikiwemo wanawake na Watoto. Kupitia programu ya LSF na wadau wake nchini, mmeweza kufanya kazi kubwa ya kusaidia jamii kupitia uwezeshaji wa kisheria,” amesema Hanifa.

Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Agness Mkawe, ametoa wito kwa washiriki wa mkutano huo, kutii matakwa ya kisheria wakati programu hizo zinatekelezwa na kwenye uendeshaji wa taasisi au mashirika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria Tanzania.

“Kupitia mkutano huu ningependa kuwakumbusha kuendelea kutii sheria, najua waliopo katika mkutano huu ni wakurugenzi ambao ndiyo watendaji wakuu wa taasisi zenu. Niwaombe kutii sheria zote kama inavyotakiwa. Kuzingatia sheria zilizowekwa inarahisisha utendaji wenu kwakuwa inasaidia taasisi zenu kutambulika na mamlaka mbalimbali za kiserikali,” amesema Wakili Mkawe.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng’wanakilala, ametoa wito kwa wadau hao kufanyia kazi yale yaliyojadiliwa katika mkutano huo.

Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Agness Mkawe

“Nafurahi kukutana na wadau wetu wakubwa, ambao mmekuwa mkifanya kazi kubwa ya kutekeleza programu yetu ya upatikanaji haki nchi nzima. Naona fahari kuona kuwa LSF sasa imetimiza miaka 10 tangu ianze kutekeleza programu yake,” amesema Ng’wanakilala na kuongeza:

“Na kupitia mashirika wanufaika wake tumefikia mfanikio mbalimbali ya sekta ya msaada wa kisheria. Naamini kuwa baada ya kikao hiki kazi yetu itaendelea kwa kasi zaidi ili kuwa na jamii iliyowezeshwa kisheria kupitia huduma bora za msaada wa kisheria,” amesema Lulu Ng’wanakilala.

Mkutano ulijumuisha washiriki takribani 200 ikiwemo watendaji wakuu wa mashirika ya watoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria kutoka mikoa yote nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria kutoka Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Visiwani Zanzibar, Hanifa Ramadhan Soud

Vilevile mkutano huu uliojumuisha mashirika wanufaika wa mradi wa uwezeshaji kisheria katika maeneo ya mijini (Urban Legal Empowerment Grantees) pamoja na wadau wengine muhimu kutoka katika sekta ya msaada wa kisheria nchini Tanzania.

Katika mkutano huo uliohusisha wadau hao kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, walijadili kuhusu matokeo ya programu hiyo iliyozinduliwa na Msajili wa NGO’s Tanzania, Vickness Mayao, tarehe 20 Agosti 2021, pamoja namaandalizi ya utekelezaji wa mpango mkakati mpya wa LSF wa miaka mitano unaotarajiwa kuanza 2022 hadi 2026.

error: Content is protected !!