Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko LSF, wadau wajadili utekelezaji mpango upatikanaji haki
Habari Mchanganyiko

LSF, wadau wajadili utekelezaji mpango upatikanaji haki

Spread the love

SHIRIKA lisilo la kiserikali linashughulika na masuala ya msaada wa kisheria nchini, Legal Service Facility (LSF)kwa kushirikiana na wadau wa sekta hiyo zaidi ya 400, wamekutana kwa ajili ya kutathimini namna ya utekelezaji programu ya upatikanaji haki nchini katika kipindi cha mwaka 2022/23. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

LSF pamoja na wadau hao kutoka katika mashirika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria 200, wamekutana katika mkutano wa siku tatu ulioanza leo Jumatano, hadi Ijumaa, ya tarehe 21 Oktoba 2022, jijini Dodoma.

Akizungumzia mkutano huo, Meneja Programu kutoka LSF, Wakili Deogratius Bwire, amesema wadau watajadili mafanikio, changamoto na mipango mikakati kwa ajili ya utekelezaji wa program hiyo, katika mwaka ujao.

Aidha, Bwire ameongeza mkutano huo utawezesha wadau wa LSF, ambao ni mashirika nufaika wa program hiyo, kutoa mrejesho wa utekelezaji wa shughuli za msaada wa kisheria, kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu mbalimbali kwa ajili ya kujijenga na kujiimarisha kwenye masuala yote yanayohusu huduma za msaada wa kisheria.

“Natoa wito kwa washiriki wa mkutano kuzitumia siku za mkutano kikamilifu., ni matuamini yangu kikao hiki kitajadili na kutoka na mapendekezo, mikakati ya utekelezaji ili kuongeza tija na kuboresha ubora wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria ili kupata matokeo chanya katika jamii,” amesema Bwire na kuongeza:

“Hii ni muhimu kwetu kama wasimamizi wa ruzuku tunazozitoa kutoka kwa wadau wetu wakubwa ambao ni Shirika la Kimataifa la Maendeleo la nchini Denmark (DANIDA). Ili kujenga jamii iliyowezeshwa kisheria.”

Naye Mwakilishi wa Msajili wa Huduma za Msaada wa Kisheria, kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Wakili wa Serikali, Agnes Mkawe, ameipongeza LSF kwa kuandaa mkutano huo kwa kuwa unalenga kuleta ustawii kwenye sekta ya msaada wa kisheria.

 “Tunaomba ushirikiano huu uendelee zaidi na zaidi katika kuhakikisha huduma ya msaada wa kisheria unaotolewa unakuwa wenye tija na manufaa kwa umma wa Watanzania. Sisi kama Serikali pia tunawashukuru wadau wa maendeleo kama Shirika la Kimataifa kutoka Denmark (DANIDA) kwa kuwawezesha LSF, ili waweze kutekeleza programu yao, ambayo imekuwa ni muhimu kwa wananchi wengi,” amesema Mkawe.

Katika hatua nyingine, Mkawe ameyataka mashirika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria kujisajiri katika mfumo wa kielektroniki, ili yaweze kutambulika, ambapo amesema kati ya mashirika 1,047, mashirika 220 ndiyo yaliyojisajiri.

“Hii inatia doa sana sana kwa sekta hii ndogo ya msaada wa kisheria ambayo ni mtakumbuka kwa kuwa awali ilidaiwa kuwa ada ya usajili wa Wasaidizi wa Kisheria ilikuwa kikwazo kwa usajili. Serikali, kwa usikivu wake, na kwa kutambua hali halisi ya mazingira mnayofanyia kazi, iliondoa takwa hili ambalo kimsingi ilikuwa katika mamlaka ya Waziri,” amesema Mkawe.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

error: Content is protected !!