Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lowassa, Sumaye, wabunge wa Chadema wammaliza Mtulia
Habari za SiasaTangulizi

Lowassa, Sumaye, wabunge wa Chadema wammaliza Mtulia

Spread the love

EDWARD Lowasa Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ameawambia wananchi wasipopigania Demokrasia watakuwa kwenye kibano. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Musipokuwa na Demokerasia mwafaa” amesema Lowassa.

Hayo ameyaeleza leo alipokuwa katika ufunguzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) za ubunge katika jimbo la Kinondoni.

Lowassa aliyekuwa Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ameeleza kuwa anaamini kuwa uchaguzi ule alishinda na kwamba hana shaka uchaguzi mwengine atashinda kwa kishindo.

Akimnadi kumgombea ubunge kwenye jimbo hilo, Salumu Mwalim amesema kuwa wasisumbuke hata kusema kuhusu mgombea aliyeshindwa kuongoza isipokuwa wapige kura kwa Mwalimu ambaye anamfahamu kuwa kijana mwenye ufanisi na mweledi kwenye shajara ya uongozi.

Naye Salumu Mwalimu aliomba kura za wananchi wa kinondoni na kuwaahaidi kuwa atafanya kazi ya kutatua changamoto zinazowakabili ikiwa pamoja na Barabara, Afya pamoja na elimu.

Amezitaja Kata nne pekee zenye zahanati kati ya kata kumi za jimbo hilo ambapo ameeleza kuwa kuna shida ya afya na upande wa elimu ameeleza kuwa Kata ya Kinondoni haina shule ya sekondari ambapo yeye anaweza kutatatua changamoto hizo.

Kwa wakati mwengine viongozi mbalimbali wa Chadema pamoja na ukawa waliwaeleza wananchi kuwa wasimchague Maulidi Mtulia kutokana na kushindwa kuwatumikia.

Fredrick Sumaye Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani ameleeza kuwa kazi ya mbunge sio kumtetea Rais ni kuwatetea wananchi kwa hiyo watu wanaohama chama kwa sababu Rais ametenda jambo jema huelewi maana ya kuwa mbunge na huelewi kazi ya mbunge.

Sumaye kuwa wafuasi wa CCM waache kutafuta sababu sizizo za msingi pamoja na kusema kwamba Salumu Mwalim ni Mzanzibari hastahili kugombea ambapo sio kweli na ni kinyume na katiba ya Tanzania.

Ameeleza kuwa CCM kimawadharau wananchi kwa kuwarejeshea mtu aliyejiudhuru ubunge ilhali amepoteza  pesa nyingi za walipa kodi ambazo zingeweza kutumika kwenye matumizi mengine ya kimaendeleo.

”Katiba inaturuhusu wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru…. leo ukitoa maoni yako unaambiwa mchochezi ambapo wabunge wetu wapo kwenye kesi kutokana na hayo.”

“Leo tunapobana mfumo wa vyama vingi tunakuwa kwenye mfumo kwenye makaratasi lakini kiuhalisi kuna mfumo wa chama Kimoja,” amesema Sumaye.

Saed Kubenea Mbunge wa jimbo la Ubungo ambaye pia ni Meneja wa Kampeni za Mgombea, amesema Mtulia alipokuwa mbunge alikopa Sh. 590 milioni na baadaye kujuizuru na kutaka kurejea tena kwa lengo la kutaka kujinufaisha.

Amesema kuwa Mwalim anatosha kuwa mbunge kutokana na historia yake ya kupambana kwa ajili ya haki za binadamu alipokuwa Mwandishi wa habari.

Ameeleza kuwa Mwalimu ni mmoja kati ya waandishi wa chache wenye kusimamia jambo analoliamini.

Makongoro Mahanga Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Ilala amewataka wananchi kukataa biashara ya kisiasa kwa kuacha kukichagua CCM.

Naye Joseph Haule Mbunge wa Mikumi, amesema ametumwa na watu wa Mikumi kuwapa ujumbe wa kutomchagua Mbunge aliyejiuzuru kwani amewadharau.

Suzan Lymo Mbunge wa viti maalumu amesema Mtulia ameamua kujiuza hivyo hastahili kuchaguliwa tena.

Marudio ya  uchaguzi wa jimbo moja unaghalimu shiling bilion moja ambazo zingeweza kutumiwa kutumiwa kwenye masuala ya maendeleo.

Easter Matiko Mbunge wa Tarime Mjini amesema mwaka 2015 wananchi wa Kinondoni tulifanya makosa kwa kumchagua Mtulia  kwa huruma ya Mungu amesaidia mbunge huyo amejiuzuru ili wananchi wa Kinondoni wapate kiongozi imara.

Patric ole Sosopi Mwenyikiti wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha), amesema kuwa Baraza hilo litahakikisha kuwa Mwalim anakuwa mbunge.

Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria Ezekia Wenje ameshangazwa na kitendo cha Mtulia kukubali kununuliwa.

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema hakuna sababu ya kuchagua CCM kutokana na hali ya maisha ya Watanzania .

”Tunapokuja kuomba kura Salum Mwalimu awe Mbunge hatumtafuti ajira ni kusafisha njia ya Demokrasia.

”Watakuja na sukari…. unakula kwa wajinga unapiga kura kwa wajanja,”amesema Lema.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameleza kuwa Mtulia amefanya dhambi itayoighalimu kizazi chake.

”Twendeni tukaionyeshe CCM kwamba Mtulia alikuwa mbunge kwa sababu ya umoja wa Ukawa”

Rechard Tambohiza akimnadi Mwalim amesema kuwa anakijua vizuri chama cha Wananchi CUF hawakuweka Mgombea isipokuwa CUF iliyoweka Mgombea ni ile inayotambuliwa kama Mungiki (wasaliti).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

error: Content is protected !!