Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lowassa, Sumaye kunguruma Dar kesho
Habari za SiasaTangulizi

Lowassa, Sumaye kunguruma Dar kesho

Spread the love

MAWAZIRI wakuu wawili wastaafu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano –Fredrick Sumaye na Edward Lowassa – kesho Jumamosi, wanatarajiwa kunguruma jijini Dar es Salaam. Anaripoti Saed Kubenea… (endelea).

Sumaye na Lowassa, watanguruma jijini Dar es Salaam, kupitia mkutano wa hadhara wa kufungua kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge, katika jimbo la Kinondoni.

Taarifa zinasema, wanasiasa hao wawili, wataongoza maelfu ya wananchi wa Kinondoni na vitongoji vyake, katika mkutano huo wa hadhara, kuanzia majira ya saa 10 jioni.

Uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam, unafanyika kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wake, Maulidi Said Mtulia.

Mtulia aliyeshinda kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa “mbinde,” kupitia Chama cha Wananchi (CUF), alitangaza kujiuzulu wazifa huo, tarehe 2 Desemba mwaka jana.

Alisema, amefikia uamuzi huo wa kujiuzulu ubunge na uanachama wake ndani ya CUF, kwa kile alichoita, “kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli katika kutekeleza mambo mengi ambayo upinzani uliahidi kufanya.”

Katika barua yake ya kujiuzulu, Mtulia alisema amechukua uamuzi huo kwa utashi wake na bila kushinikizwa na yeyote. Siku moja baada ya kujiuzulu, Mtulia alitangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema, “…nimeamua kujiuzulu nafasi zangu zote ndani ya CUF ili kuweza kuungana na Rais Magufuli. Nichukue nafasi hii, kuwaahidi wananchi wa jimbo la Kinondoni kuwa nitaendelea kushirikiana nao kama kawaida katika kuwaletea maendeleo.”

Alidai kuwa katika kipindi chake cha miaka miwili ya ubunge, amebaini kuwa serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani tuliahidi kuyatekeleza.”

Katika uchaguzi huu, CCM wamemrudisha tena Mtulia kuwania nafasi hiyo; huku Chadema inayoungwa mkono na CUF inayoongozwa na Maalim Seif Shariff Hamad, ikimsimamisha Salum Mwalimu Juma.

Mtulia ni mbunge wa kwanza katika historia ya Bunge la Tanzania, kujiuzulu ubunge na kutaka kugombea tena nafasi hiyo ndani ya muhura mmoja.

Mbunge mwingine aliyefuata nyayo za Mtulia, ni aliyekuwa mbunge wa Siha (Chadema), Dk. Godwin Ole Mollel.

Dk. Mollel ajiuzulu nafasi hiyo pamoja na uanachama wake wa Chadema, tarehe 14 Disemba 2017. Katika uchaguzi huu mdogo, Dk. Mollel anawania tena nafasi hiyo kupitia CCM.

Taarifa zinasema, kama ilivyo kwa Mtulia, Dk. Mollel naye amenukuliwa akisema, “huu ni uamuzi wangu mwenyewe. Nimeufanya nikiwa na akili timamu na bila kushinikizwa na mtu yeyote.”

Kampeni za Chadema katika jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro, zilifunguliwa leo na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Kwa mujibu wa habari ndani ya Chadema, Lowassa na Sumaye, nao wamepangiwa kuhutubia mkutano katika jimbo hilo.

Katika uchaguzi wa Kinondoni, Sumaye ndiye aliyekabidhiwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya uchaguzi huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!