December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lowassa : JK ameuharibu uchumi wa nchi

Edward Lowassa (kushoto) akiwa na Jakaya Kikwete enzi za ujana wao

Spread the love

EDWARD Lowassa, mgombea urais wa Chadema amesema, Rais Jakaya Kikwete ameharibu uchumi wa Tanzania. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Akizungumza na wafuasi wa Chadema pia UKAWA katika ofisi za Chadema mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho amesema, “rafiki yangu Jakaya Kikwete ameuharibu uchumi wa nchi yetu,” ameongeza:

“Wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani kilo ya sukari ilikuwa Sh. 600 leo ni Sh. 2,300. Mchele ulikuwa Sh. 550 leo ni Sh. 2,300. Sembe ilikuwa Sh. 250 leo ni Sh. 1,200.”

Aidha Lowassa amesema, katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete ndipo Tembo na kila aina ya wanyama wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania.

“Katika utawala wa Rais Kikwete, Tembo wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia duniani kote.

“Kila aina ya mnyama ameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu. Nitaijenga serikali yenye uchumi kwa speed (kasi), ambaye hawezi akae pembeni,” amesema Lowassa.

error: Content is protected !!