August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lowassa, Maalim, Kingunge wateta

Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar (2010-2015) (wakwanza) akiteta jambo na Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa

Spread the love

EDWARD Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania (2005-2008), Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar (2010-2015) pamoja na mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru wamekutana jijini Dar es Salaam na kujadili hali ya kisiasa hapa nchini, anaandika mwandishi wetu.

Lowassa ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF Taifa wamekuwa wakikutana mara kwa mara tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana ambao Lowassa alikuwa mgombea urais wa Tanzania huku Maalim akiwa mgombea urais visiwani Zanzibar.

Wanasiasa hao walikutana jana na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kushiriki katika uchaguzi mdogo wa marudio katika kata 22 nchini na Jimbo la Dimani lililopo Unguja, Zanzibar unaotarajiwa kufanyika hapa nchini tarehe 22 Januari, 2017.

Wengine waliohudhuria katika mazungumzo hayo ya faragha ni Julius Sunday Mtatiro, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF Taifa, Juju Danda, Katibu Mkuu wa NCCR-MAGEUZI na Balozi Musinga Bandora.

Taarifa iliyotolewa na Mbarala Maharagande, Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano wa CUF Taifa haikueleza kama kikao hicho kilikuwa ni kikao rasmi cha viongozi wa vyama vya Muungano wa Katiba ya wananchi – Ukawa au la.

error: Content is protected !!