July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lowassa kusaka wadhamini

Mgombea Urais wa UKAWA, Edward Lowassa (kulia), akiwa na mgombea mwenza wake, Juma Duni Haji.

Spread the love

MTEULE wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa atakutana na maelfu ya wanachama wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika mikoa mbalimbali wakati akitafuta wadhamini. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Katika safari hiyo, Lowassa atakutana na wadhamini wake ikiwa ni pamoja na kufanya nao mazungumzo na baada ya hapo atakuwa na kazi ya kusalimiana na wananchi.

Lowassa pamoja na mgombea mwenza wake Juma Duni Haji wanatarajia kuanza safari hiyo Agosti 14 mwaka huu.

Utambulisho huo utafanyika katika baadhi ya mikoa hiyo ambayo haijaorodhoshwa ikiwa ni hatua ya awali kabla ya kufunguliwa kwa pazia la kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu.

“Lowassa na mgombea mwenza Juma Duni Haji wataanza safari ya kwenda mikoani Agosti 14 mwaka huu” amesema Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu na kuongeza;

“katika safari hiyo atakutana na maelfu ya wanachama ikiwa ndio mwanzo wa kutambulishwa kama mgombea kupitia Chadema na pia mwakilishi wa UKAWA.”

Mwalimu amesema, kazi iliyopo kwa sasa ni kujipanga katika hatua mbalimbali kukahikisha hatua ya uchukuaji fomu wa Lowassa unafanyika bila tatuizo lolote.

Pamoja na hivyo kiongozi huyo wa Chadema amesema, amepata mialiko mbalimbali inayohitaji kukutana na Liowassa na kwamba, taratibu zinaendelea kufanyika ndani ya chama hicho.

“Hadi sasa bado hatujapanga kwamba atazunguka katika mikoa mingapi kutokana kwamba kila mkoa unamuhitaji,” anasema na kuongeza;

“Lakini baada ya kukutana na wadhamini Lowassa ataanza kampeni rasmi na atazunguka mikoa yote kama alivyoahidi siku alipoteuliwa,” anasema Mwalimu.

Lowassa alijiengua kutoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya jina lake kuondolewa katika hatua za awali kutokana na kile alichokiita kufanyiwa mizengwe ndani ya chama hicho.

Hatua hiyo ilizua mjadala ndani na nje ya chama hicho. Kutokana na kutoridhika na hatua hiyo, Lowassa aliamua kuhama na kujiunga Chadema.

error: Content is protected !!