June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lowassa kuiteka tena Dar kesho

Spread the love

MGOMBEA urais wa Chadema na anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa anatarajia kuliteka tena Jiji la Dar es Salaam kesho Septemba 20 katika mikutano mitatu. Anaandika Charles William … (endelea).

Lowassa anarejea tena jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mikutano kwenye majimbo ya Kawe na Kibamba Septemba 7 mwaka huu na kunadi wagombea wa majimbo hayo.

Lowassa alimnadi John Mnyika wa Kibamba na Halima Mdee wa Kawe kabla ya kuelekea visiwani Zanzibar katika uzinduzi wa Kampeni za Urais za Maalim Seif wa CUF.

Jijini Dar es Salaam kesho Lowassa anatarajia kufanya mikutano yake katika Jimbo la Ukonga, Kigamboni na jimbo jipya la Mbagala ambapo maandalizi tayari yamekamilika.

Lowassa ataanzia Jimbo la Kigamboni saa 3:00 asubuhi, saa 6:00 mchana atakuwa katika Jimbo la Mbagala na atamalizia kwenye Jimbo la Ukonga saa 9:00 alasiri.

Sambamba na viongozi wengine Lowassa ataambatana na timu nzima ya kampeni ya UKAWA akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye; aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja; meneja wa kampeni John Mrema pamoja na mwenyekiti wa Chadema-Taifa, Freeman Mbowe.

Lowassa anaingia Dar es Salaam akiwa tayari amezunguka kwenye mikoa 15 ya Tanzania ikiwemo Dodoma, Geita, Kagera, Geita, Shinyanga na Iringa huku mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Arusha na mingeneyo ikiwa bado kufikiwa.

error: Content is protected !!