August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lowassa: JPM ameshindwa

Spread the love

EDWARD Lowassa, aliyekuwa mgombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema, Rais John Magufuli ameshindwa kutekeleza ahadi zake, anaandika Faki Sosi.

Amesema kuwa, kilichotarajiwa na wananchi kwenye utawala wake sicho anachokifanya na kuwa, matokeo yake yamekuwa ni maisha magumu kwa wananchi huku ajira zikiota mbawa.

Ametoa kauli hiyo jana ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kufanyika Uchaguzi Mkuu tarehe 25 Oktoba mwaka jana na baadaye Tume ya Uchaguzi nchini (NEC) kumtangaza Dk. Magufuli kuwa mshindi.

Lowassa kwenye uchaguzi huo alishika nafsi ya pili kwa kupata kura 6,072,848 ambapo Rais Magufuli alitangazwa kushinda kwa kupata kura 8,882,935.

Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye aliungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwenye uchaguzi huo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema, maisha yamezidi kuwa magumu katika utawala wa Rais Magufuli.

Akitoa tathmini ya mwaka mmoja wa Rais Magufuli madarakani Lowassa amesema, Watanzania walikuwa na matarajio ya kuwa na elimu bora, ajira na uchumi jambo ambalo halijafanyika mpaka sasa.

Amesema kuwa, pamoja kuwepo na ahadi nyingi za Rais Magufuli katika nyanja mbalimbali lakini kinachofanyika sasa sicho kile kilichoahidiwa kwenye kampeni zake.

Ametoa mfano kuwa, pamoja na kuahidia elimu bure lakini inayotolewa kwa sasa sio ile iliyoahidiwa na kwamba, ukosefu wa ajira umeendelea kuwa bomu linalosubiriwa kulipuka.

“Pamoja na kuwepo kwa mafanikio katika baadhi ya maeneo, maisha yamekuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiriwa kulipuka,” amesema Lowassa ana kuongeza “elimu bure iliyoahidiwa sio inayotolewa.”

Amesema kuwa, kuwepo kwa ugumu wa maisha kumesababisha shughuli za kiuchumi kuwa ngumu jambo ambalo limewasukuma wafanyabiashara kufikia uamuzi wa kupunguza watumishi ili kukabiliana na hali hiyo.

Hata hivyo, ameonesha kukerwa na hatua ya serikali kukamata na kuwaweka ndani viongozi wa kisiasa hususani wa vyama vya upinzani.

Amesema kwamba, anapotazama nyuma kwenye uchaguzi huyo, anafarijika kuwaongoza Watanzania kupiga kura na kuungwa mkono jambo ambalo limeonesha matumaini makubwa kwao.

“Naamini nilileta sura na msisimko katika siasa za Tanzania. Nilishirikiana na viongozi wenzangu kuionesha nchi demokrasia maana yake nini?

“Ninapogeuka nyuma na kuiangalia siku ile, nasikia faraja kubwa sana hasa kwa jinsi Watanzania walivyotuunga mkono.”

error: Content is protected !!