July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lowassa hakieleweki

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa

Spread the love

KATIKA mazingira yanayoonesha Edward Ngoyai Lowassa kutojiamini, ameahirisha kukutana na waandishi wa habari katika dakika za mwisho. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).

Leo saa 5:00 asubuhi, Lowassa alitarajia kukutana na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam ili kuzungumza nao.

Taarifa ya Lowassa kukutana na waandishi ilitolewa leo mapema kupitia kwa Katibu wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Nevile Meena.

Sababu za kuahirishwa kwa mkutano huo hazijatolewa ufafanuzi mpaka sasa na haijaelezwa ni lini na watu atafanya mkutano huo.

Lowassa ni miongoni mwa makada 38 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliorudisha fomu za kuomba ridhaa ya chama hicho kuteuliwa kugombea urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.

Hata hivyo, jina lake lilikatwa katika hatua za awali hivyo kuibua kile kilichoitwa mgogoro kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC-CCM) hasa waliokuwa wakimuunga mkono.

error: Content is protected !!