Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Lowassa atunukiwa tuzo, mwanae asema…
Habari Mchanganyiko

Lowassa atunukiwa tuzo, mwanae asema…

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowasa, ametunukiwa Tuzo ya Baraza la Mawaziri wa Maji Afrika (AMCOW). Anaripoti Mwandishi Wetu, Senegal … (endelea).

Tuzo hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 22 Machi 2022 jijini Dakar, Senegal na Waziri wa Maji wa Nigeria, Suleiman Adam ambapo imepokelewa na Fredrick ambaye ni mwanae.

Fredrick akizungumza kwenye baraza hilo ambalo baba yake ni miongoni mwa waasisi wake, alisema “niko hapa leo kupokea tuzo kwa niaba ya baba yangu, ni bahati mbaya hayuko vizuri kwa sasa, amelazwa hospitali lakini tunaamini kwa maombi yenu ataamka tena na kulitumikia taifa lake.”

Amesema, baba yake kipaumbele chake kikuu kilikua maji na elimu, jambo lililomsukuma kwenye wakati wake akiwa kama Waziri wa Maji kwenda Nnchini Misri kupigania matumizi ya maji ya ziwa viktoria kwa wote ili kukomboa wakina mama ambao leo hii kwa jitihada hizo zaidi ya vijiji 500 kanda ya ziwa ni wanufaikaji wa maji hayo.

“Baba yangu angekuwa hapa leo naamini angekuwa na mengi ya kuzungumza na wenzake juu ya safari yao ya miaka hii 20 ya (AMCOW).”

“Mimi nikiwa Mbunge wa Monduli kwa sasa, ambapo baba yangu alikuwa mbunge kwa miaka zaidi ya 20, ambapo aliapa kuwaletea maji wana Monduli, ADB (Benki ya Maendeleo ya Afrika) ilitoa msaada uliosaidia sana,” amesema Fredrick

“Lakini kutokana na hali ya Monduli, bado kina baba na kina mama wanatembea umbali mrefu kutafuta maji.”

Mbunge huyo amesema “Niseme hapa leo, Monduli inahitaji AMCOW, Tanzania inataka AMCOW na Afrika inataka AMCOW.”

1 Comment

  • Monduli hakuna maji!
    Yale maji ya Mto Themi yaliyovutwa Monduli yamekwenda wapi?
    Monduli kuna maji ila nyinyi hamuwi watundu wa kuyatafuta hapohapo au ni wazi wavivu. Kila kitu mnasubiri serikali kuu!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

error: Content is protected !!