Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lowassa atiwa mbaroni Geita
Habari za SiasaTangulizi

Lowassa atiwa mbaroni Geita

Edward Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, akisalimiana na wananchi mkoani Kagera, alipohudhuria misa ya kuwaombea wahanga wa tetemeko
Spread the love

EDWARD Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita akituhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali, anaandika Charles William.

Lowassa amekamatwa alasiri ya leo baada ya kukatiza kwa mguu katika eneo stendi ya mabasi Geita, ambapo wananchi wengi walimzunguka wakimsalimia na kusababisha msongamano mkubwa wa watu, kila mtu wakitaka kumsogelea.

Hata hivyo taarifa zaidi kutoka mkoani Geita zimeeleza kwamba, mbali na Lowassa kukamatwa lakini pia baadhi ya waandishi wa habari walipigwa na kukamatwa na askari waliofika eneo la tukio kumkamata Lowassa.

“Askari walifika wakiwa katika magari matatu huku wakiwa wamejihami kwa silaha za moto, wamewapiga waandishi wa habari na kumkamata Lowassa ambapo wamempeleka Kituo Kikuu cha Polisi Geita,” kimeeleza chanzo chetu.

Khamis Mgeja, mmoja kati ya watu waliokuwa wameambatana na Lowassa katika msafara huo amesema, Lowassa alikuwa akielekea sokoni kununua matunda na kwamba wanashangaa kwanini Polisi wamemkamata.

“Alikuwa anapita sokoni kununua matunda, watu wakajazana kumsalimia na yeye kama mtu muungwana akawa akisalimiana nao, polisi wakafika kumkamata na wamempeleka kituo kikuu cha polisi,” amesema kwa simu Mgeja alipozungumza na MwanaHALISI Online.

Taarifa zaidi kuhusu tukio hili zitakujia kwa kadri tutakavyokuwa tukipokea…

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!