Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lowassa amtia majaribuni JPM
Habari za SiasaTangulizi

Lowassa amtia majaribuni JPM

Edward Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema (mwenye suti nyeusi katikati) akiingia kanisani tayari kwa misa ya kuombea walipopatwa na tetemeko la radhi
Spread the love

WAKATI Rais John Magufuli akigoma kutambua hali ya upungufu wa chakula na baa la njaa kwa baadhi ya maeneo nchini, Edward Lowassa anamtia majaribuni, anaandika Faki Sosi.

Lowassa, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema mwaka 2015 ameungana na viongozi wa dini na wanasiasa nchini katika kile kinachoonekana kuwepo kwa mwelekeo mbaya wa upatikanaji wa chakula nchini na kutaka tahadhari ichukuliwe.

Taasisi ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) zimewataka waumini wao kuomba mvua kutokana na baa la nja nchini.

“Serikali imesema haitoi chakula, mimi nimejadiliana na chama changu tumeona tufanye mpango wa kuwatafutia chakuwa Watanzania.

“Hata kama ni kutoka nje ya nchi ninaamini dunia itatusiia,” ameeleza Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu kwenye mkutano wa kampeni za Udiwani Bukoba.

Kauli ya Lowassa na viongozi wa dini inakwenda kinyume na ile aliyoitoa Rais John Magufuli alipokuwa mjini Bariadi mkoani Simiyu ambapo alisema, suala la kuwepo kwa njaa ni uzushi na kwamba, yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za njaa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Kwenye mkutano huo Rais Magufuli alidai taarifa za kuwepo kwa njaa zinasababishwa na wafanyabiashara ambao wamezoea pale panapokuwepo na ukame wanatumia vyombo vya habari kudai kuwepo njaa.

“Wapo wafanyabiashara wengine wachache waliokuwa wamezoea panapotokea matatizo kidogo tu ya ukame wanatumia vyombo vya habari ikiwa pamoja na magazeti wanayoyaamini wao sio magazeti yote, pamoja na baadhi ya wanasiasa kuzungumza Tanzania kuna njaa.

“Anayejua njaa ni Rais na sio gazeti fulani mimi ndiyo niliyepewa dhamana ya kuwaongoza Watanzania,” alisema.

Pamoja na kauli hiyo taasisi kubwa zinaeleza kuwepo kwa baa la njaa kwa baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na upungufu wa chakula nchini kutokana na kuwepo kwa ukame.

Tayari viongozi wa siasa wameeleza kuwepo kwa njaa na kuitaka serikali kuchukua hatua badala ya kuamini kinyume na hali halisi akiwemo Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.

“Kama Watanzania watakufa njaa kutokana na kutochukuliwa hatua sasa, serikali itakuwa kwenye wakati mgumu,” amesema Zitto, Mbunge wa Kigoma Mjini huku akiitaka serikali kutekeleza wajibu wake kwa wananchi.

Zitto ametoa tahadhari hiyo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni za udiwani Kijichi jijini Dar es Salaam na kwamba, wanasiasa wanatumia wasaa wa mikutano ya kisiasa iliyoruhusiwa kwa sasa kueleza hali halisi ya nchi.

Lowassa amemtia majaribuni Rais Magufuli kwa kumtaka kutafakari upya kauli yake kuhusu hali ya chakula nchini.

“Mashirika makubwa ya dini nchini yamethibitisha kuwa kuna uhaba wa chakula lakini serikali bado inaendelea kukana tatizo hilo. Narudia namuomba rais atafakari upya kauli zake kuhusu suala hili,” amesema Lowassa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!