Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lowassa amchokonoa Lissu
Habari za Siasa

Lowassa amchokonoa Lissu

Edward Lowassa
Spread the love

KITENDO cha Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania, kupitia Chadema, kuonekana kwenye televisheni na kuzunguka majimboni wakati wa kampeni zake, kimebezwa na Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho mwaka 2015. Anaripoti Mwandishi Wetu, Monduli … (endelea).

Lowassa alijiunga na Chadema Jumanne tarehe 28 Julai 2015, akiambatana na familia yake, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

Leo tarehe 24 Septemba 2020 amesema “Lissu ana maneno mengi, fujo.’

Akizungumza kwenye kikao cha ndani cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), Monduli jijini Arusha, Lowassa amemsifu aliyekuwa mpinzani wake mkubwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Dk. John Magufuli, kwamba utawala wake umefanya makubwa.

Na kwamba, amemtaka Dk. Magufuli ambaye ni mgombea urais wa CCM kutokuwa na wasiwasi wa kushinda kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

“…huko kwa kina Lissu wameanza kujipambanua sana, maneno mengi, fujo zile, wanaonekana kwenye mamitaa, maTV (televisheni), matv mengine yanatishatisha, lakini tulimwambia rais wetu, usitishike hata kidogo,” amesema Lowassa kwenye kikao hicho.

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema

Lowassa ambaye alikuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, amesema, hana mashaka na ushindi wa Dk. Magufuli na kwamba, alicho na mashaka nacho ni idadi ya kura zake za ushindi.

“Mimi sina mashaka juu ya kushinda, mashaka yangu atapita kwa kura ngapi? amesema Lowassa akisisitiza kwamba, Watanzania wengi wanamuunga mkono.

“Umma wa Watanzania uko nyuma yako na dunia inajua kwamba kuna mwanaume Tanzania. Nasema hivyo kwa sababu, Australia kama ulisikiliza BBC leo, rais anajiuzulu, kule Bolivia rais anajiuzulu, yote kwa sababu ya hii kitu, corona si mchezo,” amesema Lowassa.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Lowassa alipata kura milioni 6.07 sawa na asilimia 39.97 huku Dk. Magufuli akipata kura milioni 8.88 sawa na asilimia 58.46

Hata hivyo, Lowassa alirejea CCM tarehe 1 Machi 2019 na kupokewa na Dk. Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho, kwenye ofisi ndogo ya CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Wengine waliompokea Lowassa aliporejea CCM ni pamoja Philip Mangula (Makamu Mwenyekiti CCM-Bara), Dk. Bashiru Ally (Katibu Mkuu), Humphery Polepole (Katibu wa Itikadi na Uenezi), Kasim Majaliwa (Waziri Mkuu) na swahiba wake wa siku nyingi Rostam Aziz.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!