March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lowassa aitosa Chadema, arudi CCM

Rais John Magufuli, Mwenyekiti wa CCM akimpokea Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa aliporejea CCM

Spread the love

WAZIRI Mkuu Mstaafu wa serikali ya awamu ya nne, Edward Lowassa amerejea CCM akitokea Chadema. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Lowassa amerejea CCM leo tarehe 1 Machi 2019 na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Bashiru Ally katika ofisi ndogo za CCM jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kumpokea Lowassa, Dk. Bashiru ameeleza kuwa ujio wa mwanasiasa huyo mkongwe hapa nchini unaashiria kwamba chama hicho kinaanza kazi ya kujenga Taifa.

“Kama alivyosema Waziri Mkuu Mstaafu Lowasa amerudi nyumbani, tunaanza kazi ya kujenga taifa letu na kulinda udugu wetu ,” amesema Dk. Bashiru.

Lowassa alihama CCM katika vuguvugu la kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 baada ya kushindwa katika kura za maoni za kuwania nafasi ya kuipeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa urais, na kuipata fursa hiyo kupitia Chadema kwa mwamvuli wa vyama vinavyounda UKAWA.

error: Content is protected !!