May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lowassa afanyiwa upasuaji, alazwa ICU Muhimbili

Spread the love

 

HALI ya afya ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ni tete na amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kwa watu wa karibu na mwanasiasa huyo, zinaeleza kuwa Lowassa alilazwa Muhimbili mwishoni mwa wiki iliyopita.

Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminieli Eligaesha alipoulizwa na gazeti la RAIA Mwema jana kuhusu taarifa za Lowassa kulazwa hospitalini hapo, alisema hawezi kuizungumzia na kumtaka mwandishi azungumze na familia yake.

Habari zaidi zinasema Lowassa alifanyiwa upasuaji wa utumbo, lakini juzi alirudishwa chumba cha upasuaji baada ya mwenendo wa afya yake kuzorota.

Kwa taarifa zaidi soma gazeti la Raia Mwema. 

error: Content is protected !!