Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lowassa aeleza alivyorubuniwa Ikulu aitose Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Lowassa aeleza alivyorubuniwa Ikulu aitose Chadema

Rais John Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa walipokutana Ikulu
Spread the love

ALIYEKUWA mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa ameweka bayana kwamba wiki iliyopita aliitwa Ikulu na Rais John Magufuli na kumshawishi arejee Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Lowassa amefichua siri ya mpango huo leo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ambayo ameitoa na kusisitiza kwamba maamuzi yake ya kuhamia Chadema yalikuwa sahihi na hana mpango wowote wa kurejea CCM.

Kwa mantiki hiyo sasa Lowassa amekataa ombi la Rais Magufuli walipokutana Ikulu wiki iliyopita na kufanya mazungumzo.

Baada ya mazungumzo hao Ikulu, watu mbalimbali wakiwamo wasomi walitoa maoni yao, huku wengine wakipongeza kwenda Ikulu na wengine wakihoji ni nani aliyeomba kukutana na mwenzake.

Lowassa ameweka bayana kwamba Rais Magufuli ndiye aliyeoomba kukutana na Lowassa tofauati na watu wengine walivyokuwa wanadhani kwamba yeye ndiye aliomba kwenda Ikulu.

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia (Chadema), mwaka 2015 aligombea urais kupitia mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kutoa upinzani mkali kwa aliyekuwa mgombea urais wa CCM, Rais Magufuli.

Katika taarifa iliyotolewa na Chadema, Lowassa ameeleza “ujumbe wa Rasi Magufuli ulikuwa ni kunishawishi kutaka nirejee CCM, suala ambalo sikukubaliana nalo na nilimueleza Rais ya kwamba uamuzi wangu wa kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema haukuwa wa kubahatisha”

Wiki iliyopita, kiongozi huyo wa upinzani hapa nchini ambaye pia ni Waziri mkuu wa zamani, alikutana na Rais Magufuli Ikulu na kumsifu sana kwa kazi anayoifanya.

Kauli ya leo ya Lowassa inafungua ukurasa mpya kwa watu wanaodhani, wapinzani wengi wanaohamia CCM wanafanya hivyo kutokana na kufurahishwa na uongozi wa Rais Magufuli.

Hatua hiyo ya Lowassa iliwashangaza wengi kwani si kawaida kwa kiongozi huyo kumsifu Rais Magufuli kwani kwa muda mrefu amekuwa akikosoa utawala wake.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari, leo Januari 15, 2015, Lowassa amesema alipokutana na Rais Magufuli alimueleza masuala mbalimbali yanayowakumba wananchi na wanasiasa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.

“Nilijadiliana naye kuhusu masuala mbalimbali ya msingi kuhusu nchi yetu ikiwemo kutoheshimiwa kwa Katiba na sheria, uminywaji wa demokrasia, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

”Kupotea kwa watu, kuvamiwa, kutishwa na kushambuliwa kwa viongozi wa kisiasa wa upinzani na hali ngumu ya uchumi kwa wananchi wetu. Ni imani yangu kwamba Rais atayazingatia na kufanyia kazi masuala haya kwa masilahi yetu.”

2 Comments

 • “si kawaida kwa kiongozi
  huyo kumsifu Rais Magufuli kwani kwa muda mrefu amekuwa akikosoa utawala
  wake”
  Hapa kwa kweli mwandishi unatuzingua.

  Hatuzungumzii kwa kawaida au kwa muda mrefu. Tunazungumzia yale aliyosema kwa wanahabari nje ya Ikulu mbele ya JPM. Kwanini wakati ule asiseme haya anayosema sasa? Badala yake aliwaambia mazuri ya JPM tuuu na kumsifu tuuu. Sasa anatuambia eti alimkosoa.Kwanini alificha kusema wakati ule?

  Halafu JPM alisema ni EL ndiye aliyeomba mkutano. Kwanini EL alikaa kimya asikanushe?

  Halafu, je akiwa mjumbe wa kamati kuu alishauriana na viongozi wenzake kabla ya kujikita Ikulu? Je Mbowe alijua kabla? Kwanini aende peke yake kisirisiri?
  Halafu baada ya kutoka Ikulu kwanini asitoe risala (Press Release) yake binafsi badala ya kumuachia JPM atoe yake?
  Kamati kuu inachukua hatua gani?

  Aulizae ataka kujua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!