July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lowassa aelekea Ikulu

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akikabidhiwa fomu ya kuwania Urais na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akikabidhiwa fomu ya kuwania Urais na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Spread the love

MWANACHAMA mpya wa Chadema, Edward Lowassa, ameanza tena safari yake ya kuelekea Ikulu. Leo (Alhamisi) amechukua fomu ya kuwania urais, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaandika Hamis Mguta, DSJ … (endelea).

Lowassa alichukua uamuzi huo wa kihistoria majira ya saa 6 mchana, makao makuu ya Chadema, Ufipa, jijini Dar es Salaam. Alilakiwa na maelfu ya wanachama, washabiki na wafuasi wa kiongozi huyo.

“Tumeanza safari mpya ya matumaini na kuelekea ushindi. Sina cha kuwalipa, ispokuwa ninawaahidi kuwa nitawafanyia kazi itakayoleta ushindi,” amesema Lowassa mara baada ya kukabidhiwa fomu.

Lowassa, mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa nchini, alijiengua Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumanne iliyopita na kujiunga na Chadema, ambako anatarajiwa kugombea urais kupitia Muungano wa UKAWA.

Taarifa zinasema, ujio wa Lowassa ndani ya Chadema, utaingiza wenyeviti wa mikoa 22 kati ya 32 na wilaya 80 kutoka CCM.

Tayari aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi wa CCM, Marson Chizii, Balozi Bandora na aliyekuwa naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Godluck Ole-Medeye, wametangaza kujiunga na Chadema.

error: Content is protected !!