January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lowassa aahidi kufufua viwanda nchini

Spread the love

MGOMBEA uraisi kwa tiketi ya UKAWA, Edward Lowassa ameahidi kufufua viwanda hususan kiwanda cha General Tyre kilichopo mtaa Njiro jijini Arusha ikiwa ni njia mojawapo ya kukuza ajira na kuinua uchumi wa nchi. Anaandika Ferdinand Shayo, Arusha … (endelea).

Akizungumza katika mkutano wa kutafuta wadhamini uliofanyika jana katika viwanja vya Tindigani, jijini Arusha, Lowasa amesema anauchukia sana umaskini, ili kuondoa umaskini lazima kama nchi ikuze ajira, kwa kuanzia atafufua viwanda.

Lowassa amesema mbali na kufufua viwanda lakini pia atahakikisha anaboresha maslahi ya walimu wawe na hamasa na kufundisha ili kuwe na kizazi chenye elimu, pamoja na kuwapatia mikopo wachimbaji wadogo wadogo wa madini itakayowasaidia kupata vitendea kazi.

“Leo nimekuja kuwashukuru kwa kujitokeza kunidhamini kwa wingi, lakini nawahidi kati ya mambo nitakayoyashughulikia ni kuboresha mfumo wa elimu, kupunguza msongamano wa magari katika miji mikubwa,” anasema Lowassa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema UKAWA unalenga kuwaunganisha Watanzania wote na kuleta ukombozi wa nchi hii hivyo, amewataka wawaunge mkono juhudi hizo ili kupata ukombozi wa kweli.

Naye Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amelaani vikali tukio la polisi kupiga mabomu ya machozi katika msafara wa Lowassa wakati akitoka kiwanja cha ndege cha KIA kuelekea jijini Arusha jambo ambalo ni ukiukwaji wa haki za kidemokrasia.

error: Content is protected !!