August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

London yapata Meya Muislam

Spread the love

JIJI la London nchini Uingereza limempata Sadiq Khan ambaye ni meya wa kwanza Muislamu katika historia ya jiji hilo, anaandikaWolfram Mwalongo

Khan mwenye umri wa miaka 45 amechaguliwa kwa kura 1,300,000 ikiwa ni kiwango cha juu kuwahi kutokea kwa meya yeyote kushinda katika jiji.

Ushindi huo unaeleza kuwa ni furaha kubwa na unaondoa dhana ya kuwepo kwa ubaguzi dhidi ya Dini ya Kiislamu kwa miaka mingi.

Akitoa hotuba yake  baada ya kutangazwa mshindi  khan ameahidi kuongoza jiji hilo kwa usawa na kwa maslahi ya watu wote. Khan aliwahi kuwa waziri kupitia chama cha upinzani cha Laba.

Meya huyo anakuwa watatu tangu kuchaguliwa kwa meya wa kwanza Ken livingstone aliye shinda kama mgombea binafsi mwaka (2000-2004) baadae akajiunga na chama cha labpour nakushinda  akaongoza tena (2004-2008) ndipo alipoingia Boris Johnson  mwaka (2008-2012) akaendelea (2012- 2016) anapo mkabidhi Sadiq Khan anaye tarajiwa kuongoza kwa kipindi cham mika minne ijayo na baadae endapo atagombea tena.

error: Content is protected !!