March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Loliondo washangilia Profesa Maghembe kupigwa chini

Dk.Hamisi Kigwangalla, waziri wa Maliasili na Utalii

Spread the love

SIKU tano tangu Rais John Magufuli afanye mabadiloko kwenye Baraza la Mawaziri, wananchi wa wilaya ya Loliondo mkoani Arusha wameshangilia  kutemwa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Professa Jumanne Magembe, anaandika Faki Sosi.

Profesa Magembe alikuwa waziri wa Maliasili na Utalii ambapo kwa sasa nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto.

Moja ya sababu ya wananchi hao kufarahishwa kwa kuondolewa kwa Profesa , Magembe ni mgogoro wa ardhi eneo la pori tengefu.

Mgogoro huo wenye zaidi ya miaka 20   unawahusu wawekezaji katika eneo la hifadhi pamoja na wananchi wa Loliondo.

Wananchi hao wametoa ya moyoni kwenye  mkutano wa hadhara uliofanyika jana  kwenye eneo la kata ya Ololosokwan ambapo mara ya mwisho Waziri Mkuu,  Kassimu Majaliwa alifika huko akiwa na Profesa, Magembe pamoja Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo.

Hata hivyo wananchi hao weamesema hakukupatikana suluhisho la mgogoro huo.
Mkutano uliofanyika jana wakazi wa eneo hilo walionesha matumaini yao kwa Dk Kigwangala na kumshauri atende haki kwa wananchi.

Boniphace Kanjwel, Diwani wa Kata ya Soitsambu, amesema kuwa wao siyo waharibifu wa mazingira ni watunzaji isipokuwa wahifadhi ndiyo wanaoyaharibu.
Dk Kigwangala alishauriwa kuwa anatakiuwa kujua kiini cha kuwapo mgogoro katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 20.

“Waziri tunaomba akutane na sisi aje tumweleze kiini cha mgogoro na akitusikiliza hapa nawahakikishia hakuna mgogoro,”

“Wateule katika wizara ya maliasili na utalii wanapaswa kutambua ya kwamba ardhi wanayoipigania ni mali yao kisheria na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni uvamizi na ukiukwaji wa haki za binadamu” amesema Ndoinyo.

Nektayo Ledidi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Olorien kwa upande wake amesema wao kama jamii ya Wamasai wanaiomba serikali kutambua kwamba wao ni Watanzania wanaostahili haki ya kupatiwa makazi na siyo kunyanyaswa.

error: Content is protected !!