Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko LNG kuanza kutoa gesi 2030
Habari Mchanganyiko

LNG kuanza kutoa gesi 2030

Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni akizungumza na waandishi wa habari katika banda la mamlaka hiyo lililopo katika Viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba wilayani Temeke jijini Dar es Salaam
Spread the love

MKURUGENZI Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni amesema iwapo hakutakuwa na vikwazo, uzalishaji wa Mradi wa Kuchataka Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) katika Mkoa wa Lindi utaanza mwaka 2025 na gesi ya kwanza itaanza kuuzwa 2030. Anaripoti Selemani Msuya … (endelea).

Mhandisi Sangweni aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46 maarufu Sabasaba yanayofanyika katika Kiwanja cha Mwalimu Julius Nyerere Temeke Dar es Salaam.

Alisema kilichofanyika Juni 11 mwaka huu ilikuwa ni makubaliano ya awali ya mkataba husika, kama majadiliano ya muundo wa mradi, ukubwa wa mradi, sheria iweje na kwamba majadiliano yakikamilika wanatarajia Desemba 8 mwaka huu watasaini mkataba uliokamilika.

Sangweni ambaye ni Mwenyekiti wa Majadiliano alisema baada ya mkataba rasmi kukamilika wanatarajia kwenda kwenye kazi ya usanifu wa mradi na namna ya kupata fedha za utekelezaji.

“Tunategemea utekelezaji wa mradi huu ujenzi wake utaanza 2025 na ndani ya miaka minne hadi mitano utakuwa umekamilika na gesi ya kwanza itaanza kutoka 2030,” alisema.

Mhandisi huyo alisema iwapo hakutakuwa na changamoto katika mradi huo unaogharimu zaidi ya Sh.trilioni 70 utaweza kuzalisha gesi asilia kwa  miaka 30.

Alisema katika kipindi cha ujenzi wa mradi huo zaidi ya ajira 10,000 zitapatikana na ajira za kudumu zitakuwa zaidi 600 pamoja na kuchochea shughuli nyingine za kiuchumi kwenye eneo la mradi.

Mkurugenzi huyo alisema tafiti zinaonesha kuwa utekelezaji wa miradi mikubwa kama hiyo ikifanyika katika nchi kama Tanzania pato la taifa litaongezeka kwa asilimia 1.5.

“Huu sio mradi mdogo, wakubeza, kwani utachangia ukuaji wa uchumi kwa kasi kubwa na pato la taifa litaongezeka kwa asilimia 1.5, ndio maana timu ya Serikali hailali kuhakikisha mradi unatekelezwa,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema baada ya mradi huo kuanza kuzalisha gesi asilia wanatarajia kuuza katika nchi za Mashariki ya Mbali kama Japani, China na nyinginezo ambazo zimeonekana kuhitaji.

Aliwataka wawekezaji wa Kitanzania na wengine kujipanga vizuri katika kutumia fursa zitakazokuwepo katika mradi huo, akitolea mfano kuwa nondo, saruji na bidhaa nyingine zitahitajika.

Mwenyekiti huyo alisema watajitahidi kuandaa mazingira wezeshi ili Watanzania wawe kwenye viwango ambavyo vinakubalika katika miradi mikubwa kama hiyo.

Alisema wamekuwa wakkifanya mikutano na wadau mbalimbali kama wakuu wa taasisi waweze kujiandaa kushiriki katika mradi huo ambao unaenda kuleta mapinduzi ya kiuchumi, kijamii na maendeleo.

Mkurugenzi huyo alisema azo la mradi huo lilinza mwaka 2012 ila kuna changamoto zilizotokea, lakini kwa sasa Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuendeleza na matarajio yao ni mradi kutekelezwa kwa viwango vinavyokubalika.

Alisema kazi ya PURA ni kushauri Serikali kuhusu shughuli za mkondo wa juu,  kuthibiti na kusimamia Mradi wa LNG ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa Watanzania.

Sangweni alitoa wito kwa Watanzania kutembelea banda la PURA ili waweze kupata elimu zaidi kuhusiana na mamlaka hiyo ambayo ina kazi moja ya kuhakikisha rasilimali mafuta na gesi zinagundulika na kutumika.

1 Comment

  • Kwa nini watanzania wasitumie gesi hii?
    Kwa nini gesi igeuzwe kimiminika na kuuzwa nje mpaka iishe?
    Kwa nini hakuna sheria ya kulinda gesi yetu kabla ya kukutana na watu wa nje?
    Naona aibu tunakwenda kwenye mikutano hatujui wala kuwa na maslahi ya taifa. Sasa wao ndio wanatunga sheria ya mkataba na tunaambulia kiduchu.
    Kwa nini hatuzipi nchi zilizobobea gesi kama Urusi na Norway…serikali na serikali zikutane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!