May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Liverpool, Manchester Kumaliza ‘kiporo’ chao leo

Spread the love

 

 Mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu nchini England kati ya Liverpool na Manchester United kuarishwa kutokana na vurugu za Mashabiki wa Manchester kuandamana, hatimaye wakongwe hao watakipiga leo kwenye Uwanja wa Old Trafford majira ya saa 4 usiku. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Wawili hao wanakutana huku tayari bingwa mpya ambaye ni klabu ya Manchester City ameshatangazwa, mara baada ya Manchester United kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Leceister City.

Mchezo huu ambapo utakuwa muhimu zaidi kwa Liverpool kutokana na kugombania nafasi nne za juu ili waweze kushiliki michuano ya Ligi yaMabingwa Barani Ulaya msimu ujao.

Liverpool ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 57, na michezo 34 huku nafasi ya tano ikishikwa na Westham ikiwa na pointi 58 na michezo 35.

Nafasi ya nne inakamatwa na Chelsea mwenye pointi 64 na michezo 36, huku kwenye nafasi ya tatu akishikilia Leceister City mwenye pointi 66 na michezo 36.

Mchezo huo ambapo hapo awali ulipangwa kuchezwa tarehe 5 Mei 2021 haukufanyika kutokana na maandamano waliyoyafanya mashabiki wa klabu ya Manchester United ambao walikuwa wanashinikiza kwa wamiliki wa timu hiyo Familia ya Glazzer kuachana na timu hiyo.

error: Content is protected !!