May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Liverpool kuikabili Manchester leo, Salah, Firmino kurejea

Spread the love

MARA baada ya kupoteza kwa bao 1-0, mbele ya Burnley, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ataongoza kikosi chake kwenye Uwanja Old Trafford kuwakabili Manchester United kwenye wa mzunguko wa nne wa kombe la FA nchini England. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa hatua ya mtoani utachezwa majira ya saa 2 usiku ambapo Liverpool wanaingia kwenye mchezo huo huku wakiwa hawajapata ushindi kwenye mechi sita na kutofunga bao lolote kwenye michezo minne.

Katika mchezo wa leo washambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah na Roberto Firmino watarejea uwanjani mara baada ya kukosekana kwenye mchezo wa Alhamisi dhidi ya Burnley huku wakiendelea kukosa huduma ya beki wao wa kati Virgil Van Dijk.

Kuelewkea mchezo huo kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amefunguka kujisikia faraja kurejea kwa wachezaji hao wawili na atarajia kuwanzisha kwenye mchezo huu kwa kuwa wanahitaji ushindi.

“Huu ni mchezo wa kombe na mechi itaamuliwa usiku huu na tunahitaji kushinda,” alisema kocha huyo.

error: Content is protected !!