WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amelitaka Baraza la Habari Tanzania (MCT), kusimamia vyema vyombo vya habari ili vitekeleze majukumu yake kwa mujibu wa sheria. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Majaliwa ametoa agizo hilo leo Jumamosi, tarehe 28 Mei 2022, akizungumza katika hafla ya utoaji Tuzo Mahiri kwa Waandishi wa Habari Tanzania (EJAT2021), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Nirudie tena kutoa rai kwa MCT ongezeni jitihada katika kusimamia maadili ya taaluma yetu. Mhakikishe tunashajaisha waandishi wafanye kazi zao kwa kufuata maadili. Naamini Baraza la Habari ambalo mmelianzisha wenyewe lili liwasimamie litakuwa mstari wa mbele kuhakikisha vyombo vinatimiza majukumu yake,” amesema Majaliwa.
Aidha, Majaliwa, amewataka wanahabari kuweka mbele maslahi ya taifa kwa kutmia kalamu zao vizuzri katika kuchochea maendeleo pamoja na kuhamasisha amani na utulivu.
Katika hatua nyingine, Majaliwa amesema Serikali inayoongozwa na ya Rais Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuimarisha uhusiano wake na vyombo vya habari, huku akiwataka wanahabari kutokiuka maadili ya taalum zao ikiwemo kuchapisha ama kutangaza taarifa za uongo, ili vyombo vyao visifungiwe.
“Rais wetu ni msikivu na anaendelea kuimarisha uhusiano mwema wa vyombo vya habari, sote tunaendelea kushuhudia runinga za mtandaoni zilizokuwa zimezuiwa zikifunguliwa, lakini kama hilo halitoshi, Serikali imetoa leseni za magazeti manne yaliyokuwa yamemaliza adhabu zake,” amesema Waziri Majaliwa.
Hii ni NGO au GO? Governmental Organization! Nani kalipa gharama za Serena? Dola ngapi? Ulaji tu!!