May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

LIVE: Miaka 60 ya Uhuru, marais Afrika wajitokeza

Spread the love

 

HAPPY Birth Tanganyika. Ndiyo Tanganyika ama kwa sasa Tanzania Bara, leo Alhamisi, tarehe 9 Desemba 2021, inaadhimisha miaka 60 ya Uhuru. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ilipata Uhuru kutoka kwa Wakoloni wa Kiingereza, tarehe 9 Desemba 1961 chini ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Sherehe za maadhimisho hayo zinafanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.

Ni shehere ambazo kwa mara ya kwanza, imeshuhudia ushiriki kwa mara ya kwanza wa Jeshi la Uhamiaji.

Baadhi ya wakuu wa nchi ambazo wapo uwanjani; ni Uhuru Kenyatta (Kenya), Filipe Nyusi (Msumbiji), Paul Kagame (Rwanda), Azali Assoumani (Comoro), Dk. Hussein Ali Mwinyi (Zanzibar).

Pia, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Hafidhi Amri, mme wa Rais Samia.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

error: Content is protected !!