March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lisu kupamba tamasha la injili

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki

Spread the love

MWIMBAJI wa nyimbo za injili, John Lisu anatarajia kutikisa katika tamasha la uamsho lililoanza ambalo litashirikisha watui wote bila kujali itikadi za dini zao, anaandika Dany Tibason.

Katika mahojiano maalumu na gazeti hili Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (victory Christian center) DK. Huruma Nkone alisema wameandaa mkutano wa uamsho unaoshirikisha watu wote bila kujali utofauti wa madhehebu.

Akifafananua zaidi amesema mhubiri katika mkutano huo wa uamsho ni Askofu Yona Suleiman kutoka kiomboi mkoani Singida.

Tamasha hilo la uamsho litafanyika katika ukumbi wa Kanisa la Victory Christian Center na utafanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanakabiribishwa ili kusikia neno la Mungu ambalo litatolewa na wahubiri mbalimbali.

“Ni kwa neema na waimbaji wengine watapamba mkutano huo wa uamsho ni Rivers of Joy International Kwaya ya Kanisa la KLPT Tageta na nyingine nyingi”alieleza Dk.Nkone.

DK Nkone ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar kujitokeza kwa wingi kwani huduma ya maombi na maombezi itatolewa bure.

error: Content is protected !!