Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya
Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara, Tundu Lissu, amesema amekuja na “dawa” ya kupanda kwa bei za vitu kulikosababisha ugumu wa maisha. Anatipoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu ambaye amewasili nchini leo akitokea nchini Ubelgiji ambako alipewa hifadhi baada ya kukimbia kuhofia usalama wake, amesema matatizo yote yanasababishwa na uongozi ambao Katiba ya sasa inawapa mamlaka makubwa ya kuamua mambo.

“Tulivyotika airport nimekaa juu ya ile gari tumepita kote nimesikia maneno mengi sana ya kweli, nimesikia inakuaje bei ya maharage ipo sawa na bei ya nyama, nimesikia watu wananiambia mchele buku… wanataka bei ya mchele iwe buku nikasema duh kutokukaa nyumbani unapitwa na mengi

“Sasa hivi ndo hali ngumu, magarage hayakamatiki, mchele haukamatiki, hakuna maji hakuna umeme tozo kila mahali na wale wanaopokea mshahara makato wanayokatwa wawe polisi, makarani, manesi na walimu, makato wanayokatwa kwenye mishahara yao makato ni makubwa mno,” amesema Lissu.

Sasa nafikiria hawa watu wananiambia maneno haya wanafikiri mimi ndo mwenye mamlaka ya kushusha bei hizi… sasa mimi sina mamlaka ya kupunguza bei hizo isipokuwa kuyazungumza tu hiyo nitaifanya hiyo haihitaji niwe na kacheo fulani inahitaji nisimame kama hivi nizungumze na watanzania.

Lissu amesema maisha magumu ni tatizo la kimsingi la kisiasa, “Mungu hajasema maisha yawe magumu, kusiwe na umeme, kusiwe na maji, mtozwe tozo, hayo ni mambo ya kisiasa, kwasababu hiyo tuna mamlaka ya kuyaondoa.

“Kama umechoshwa na tozo na maonevu haya hili lipo ndani ya uwezo wetu, halihitaji maombi yale ambayo Mungu ametupa uwezo wa kuyashughulikia tusimbebeshe Mungu mzigo. Ni tatizo la kiutawala, tatizo la kikatiba kama kweli mmechoka dawa ninayowapa ni hii tutafute suluhu ya kisiasa tutafute suluhu ya kikatiba tutafute katiba mpya,” amesema Lissu.

“Kuna kamstari mahali ambako kako kwenye hii katiba kanakoelezea kwanini bei ya maharage ni sawa na bei ya nyama, kanazunguzia uwezo wa bunge wa kutunga sheria za tozo na kodi zote.

Lissu amesema mstari huo unasema Bunge halitajadili hoja au mswada au jambo lolote linalohusu fedha mpaka jambo hilo lipate ridhaa ya Rais na kuwasilishwa bungeni na waziri.

Kwa mujibu wa hayo maneno yamempa Rais “mamlaka ya kuamua utozwe kodi, ushuru na namna nyingine ya unyang’anyi wowote kadri atakavyoamua.”

Kwahiyo tunapaswa tujue tatizo ni nini, tatizo ni Katiba.

Amesema Katiba ya Tanzania kwa mujibu Baba wa Taifa imempa Rais uwezo wa kuwa dikteta

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!