November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu: Wataiba kura zangu

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amedai ushindi wake ukiwa mwembamba, ‘utapinduliwa.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Muleba … (endelea).

Amesema, kukabiliana na hilo, amewataka Watanzania kumpigia kura kwa wingi ili wapinduaji wakose mahala pa kuanzia.

“Tukishinda kwa ushindi kidogo, wale wataiba na pia tukishinda kawaida, wataiba. Sasa ili wasiibe, inatubidi tushinde kwa kura nyingi.

“Tushinde kwa kura za kimbunga ili wakose sehemu ya kuanzia kupindua. Inabidi wakute kila kituo cha kuhesabia kura kwenye jimbo, wilaya, mkoa tumeshinda,” amesema.

Mgombea huyo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa chama hicho ametoa kauli hiyo tarehe 23 Septemba 2020, kwenye kampeni zake za urais akiwa Kamachumu, Muleba mkoani Kagera.

Amesema, njia rahisi ya kuzuia kile alichoita ‘balaa’ kisitokee, ni wananchi kujitokeza kupiga kura kwa wingi tarehe 28 Oktoba 2020.

“Mwezi ujao tuzuie hili balaa, tupige kura tujikomboe,” amesema Lissu akisisitiza, kwamba kwa kufanya hivyo, itakuwa ni ukombozi kwa Taifa.

error: Content is protected !!