Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu: Tusishiriki tena uchaguzi hadi…
Habari za Siasa

Lissu: Tusishiriki tena uchaguzi hadi…

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara nchini Tanzania, Tundu Lissu, amevishauri vyama vya siasa vya upinzani nchini humo, kutoshiriki uchaguzi hadi pale mfumo wa demokrasia utakapoimarika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu ametoa ushauri huo jana Alhamisi tarehe 31 Desemba 2020, wakati anatoa salamu zake za mwaka mpya wa 2021 kwa Watanzania.

Lissu amesema, vyama hivyo vitakuwa na wakati mgumu kama vitashiriki uchaguzi bila ya uwepo wa tume huru ya uchaguzi na mfumo mzuri wa kidemokrasia.

“Itakua vigumu sana kushiriki tena uchaguzi wowote ule katika mazingira ambayo bado tuna tume za aina hii za uchaguzi, msimamo wangu binafsi tusije tukarogwa tena kushiriki kwenye uchaguzi katika mazingira haya ya tume hizi na ya mfumo huu,” amesema Lissu.

Lissu amevishauri vyama hivyo kwa kushirikiana na wananchi pamoja na Jumuiya za Kimataifa, vianze vuguvugu la kudai tume huru ya uchaguzi.

“Na hii aina maana tunyamaze tu, nimesema tuliamshe ndani ya nchi na nje ya nchi, tukabe kila mahali. Itafika mahali wataachia tu, mahali ambako wananchi wameamka pamoja na misaada ya Jumuiya za Kimataifa, inawezekana kabisa.”

“Kwa hiyo, hilo liwe jukumu letu kuanzia sasa. hakuna uchaguzi bila mfumo wa kidemokrasia wa uchaguzi,” ameshauri Lissu.

Mwanasiasa huyo aliyerejea nchini Ubelgiji baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktobs 2020 kumalizika, ametoa salamu hizo kupitia video yake aliyoisambaza mitandaoni.

Lissu aliondoka Tanzania na kurejea nchini Ubelgiji alikoishi kwa takribani miaka miwili, kwa ajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana tarehe 7 Septemba 2017 jijini Dodoma akitokea bungeni.

Mwanasiasa huyo alidai anarejea Ubelgiji baada ya kupata vitisho vya kiusalama.

 

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema

Hata hivyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro, alimuita Lissu arudi Tanzania akimuahidi kumpatia ulinzi jambo ambalo Lissu alilipinga.

Katika uchaguzi huo, Lissu aligombea kiti cha Urais wa Tanzania kupitia Chadema ambapo alichuana vikali na aliyekuwa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Dk. John Pombe Magufuli na kushika nafasi ya pili.

Matokeo yaliyotangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC), yalikipa ushindi wa kishindo CCM katika nafasi ya urais, ubunge, uwakilishi na udiwani.

CCM kilishinda urais wa Tanzania na Zanzibar pamoja na kuzoa viti zaidi ya 240 huku vyama vya ulinzani vikiambulia majimbo 6.

Chadema kilipata jimbo moja, Chama cha Wananchi (CUF) kimoja huku ACT-Wazalendo kikipata majimbo manne Zanzibar.

4 Comments

  • Asante ndugu lissu kwa habari njema lakini uwelewe wewe ndio nahodha na umejitosa bahari kabla ya dhoruba sasa tukuelewe vp ndugu lissu acha kuzidanganya fikra zako fikiria mema ambayo yatakusaidia katika maishA yako katika ulimwengu wa kisiasa wewe haupo tena nasiasa bongo zimeamia bungen hazipo tena ktk mitandao

  • Mimi sijawah kuona kiongoz wa vita hakai mstari wa vita na huku akidai anaongoza vita na anatumain kusinda! ivi kweli lisu anawaaminisha watanzania wadai tume huru wakati yeye ameikimbia tanzania kwan hiyo tume itasimamia uchaguz uberigiji? Ana matatizo lisu kwakwel

  • Mtatizo gani aliyonayo kwa mfano? Kusema anaongelea nje ya nchi, alipaswa aongelee hapahapa ni uchawi.

    Kanusurika kuuwawa hapahapa, nani kachukua hatua yoyote zaidi ya kuona tabia za kichawi zinadhihirika waziwazi? Tanzania kama kunamtu anasema hajawahi kuona uchawi waziwazi, akapimwe akili. Kipitia Tundu Antipas, tumeona wachawi wakiroga kweupe kabisa bila hofu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!