Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu: Tumemaliza kazi, mawakala msituangushe
Habari za SiasaTangulizi

Lissu: Tumemaliza kazi, mawakala msituangushe

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema
Spread the love

MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amewaomba wanachama wa chama hicho, kuwalinda mawalaka wao ili kutimiza ndoto ya kuikomboa nchi hiyo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, Lissu amejitabilia ushindi wa asilimia 70 katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika kesho Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 ukihusisha madiwani, wabunge na Rais.

Lissu amesema hayo leo Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020 katika mkutano wake wa kufunga kampeni za urais uliofanyika Uwanja vya Tanganyika Pakers-Kawe jijini Dar es Salaam.

Amesema, safari yasiku 62 ya kampeni zimemalizika kwa kuzunguka nchi nzima kuwaeleza sera mbalimbali na kile watakachokitanya baada ya kuingia madarakani endapo watapewa fursa na Watanzania.

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema

Lissu amesema, ushindi wa Chadema na Watanzania wapenda maendeleo unawategemea mawakala wa vituo zaidi ya 80,000 nchi nzima.

Amewaomba Watanzania kuwalinda mawakala hao kwa kuwa ni wachache na kazi iliyoko mbele yao ni kubwa.

“Mawakala wa vituo na mawakala wa kituo kikuu cha majumuisho hao watakua mstari wa mbele katika mapambano ya kesho, ni wachache kuliko kazi iliyoko mbele yako, tunawaomba sana wawe waaminifu,” amesema Lissu

“Wananchi nchi nzima, wakala wetu akivurugwa ingilieni kati na kunyimwa fomu hakikisheni msimamizi hatoki na fomu yetu, tuwalinde mawakala wetu ili watulindie kura zetu. Tuwaopelekee maji na chakula. Mawakala wetu tunawategemea sana katika mabadiliko ya nchi yetu,” amesema.

Halima Mdee, Mgombea Ubunge wa Kawe kwa tiketi ya Chadema

Mwanasiasa huyo amesema, utafiti uliofanywa na wataalamu wa Chadema unaonesha wanakwenda kushinda kati ya asilimia 65 hadi 70 ya waliojiandikisha kupiga kura, milioni 29 ambao watakikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Watalaamu wetu wamefuatilia na kubaini kati ya asilimia 65 hadi 70 watapiga kura kuikataa CCM. Wanatuambia licha ya wagombea wetu wa ubunge na udiwani kuenguliwa bado kesho tuna uwezo wa kuwa na wabunge wengi zaidi kuliko CCM.”

“Wanasema kwamba, idadi ya wapiga kura waliojiandikisha idadi ya jumla ya wabunge kwa wagombea wetu itakua kubwa kukilo CCM karibu asilimia 60 hadi 70 itakuwa upande wetu,” amesema Lissu.

Kati ya majimbo 264 ya uchaguzi wa wabunge, CCM imekwisha kujikusanyia majimbo 28 baada ya wagombea wao kupita bila kupigwa.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!